IQNA

Sudan

Nakala ya Qur'an yabakia salama baada ya gari kuteketea moto Sudan + Video

17:22 - January 29, 2024
Habari ID: 3478271
IQNA - Nakala ya Qur'an Tukufu ilibakia salama baada ya moto kuteketeza gari nchini Sudan hivi karibuni.

Gari hilo lilishika moto wakati wa mapigano yanayoendelea katika nchi hiyo ya Kiafrika, tovuti ya al-Naylayn iliripoti.

Baada ya kuzimwa, nakala ya Qur'ani Tukufu ilipatikana kutoka kwenye gari ikiwa salama.

Wakati kila kitu kwenye gari kikiteketezwa, Msahafu huo ulionekanya ukiwa umesalia salama. Kulikuwa na uharibifu kidogo kwenye jildi lake

Takriban watu 13,000 wameuawa katika vita vya Sudan vilivyozuka Aprili 15, 2023, kulingana na makadirio ya hivi karibuni ya Umoja wa Mataifa.

Sudan ilikumbwa na vita kati ya Jeshi la Kitaifa, linaloongozwa na Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, ambaye ni mkuu wa Baraza tawala la nchi hiyo, na kundi la wanamgambo wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) tangu Aprili 2023.

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imetangaza hivi karibuni katika taarifa yake kwamba, "Takriban watu milioni 7.6 wamekimbia makazi yao ndani na nje ya Sudan tangu mapigano yazuke."

Kulingana na ofisi ya Umoja wa Mataifa, zaidi ya visa 9,700 vinavyoshukiwa kuwa kipindupindu, vikiwemo vifo 269 vinavyohusishwa, viliripotiwa nchini Sudan kufikia Januari 16.

Kamanda wa Vikosi vya Radiamali ya Haraka vya Sudan (RSF) Jenerali Mohammad Hamdan Dagalo (Hemedti) anasisitiza kuwa njia bora ya kuhitimisha mapigano nchini humo ni kuviunganisha vikosi hivyo na Jeshi la Sudan.

3487000

captcha