IQNA

Qarii na hafidh maarufu wa Qur'ani Sudan apoteza maisha katika ajali + Video

16:50 - November 07, 2020
Habari ID: 3473336
TEHRAN (IQNA)- Qarii na hafidh maarufu wa Qur'ani Tukufu nchini Sudan, Sheikh Noreen Muhammad Sidiq amefariki katika ajali barabarani.

Waziri wa Masuala ya Kidini na Wakfu Sudan Nasruddin Mufreh ametuma ujumbe kupitia ukurasa wake wa Facebook na kuandika kuwa Sheikh Sidiq alifariki katika ajali ya barabarani akiwa na maqarii wengine watatu wa Qur'ani.

Watatu hao wametambuliwa kuwa ni Ali Yaqub, Ewaz al Karim na Muhnad al Kinani ambao wote walikuwa wamehifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu. Aidha amesema qarii wa Misri, Sayyid bin Omar, pia alikuwa katika gari moja na wenzake Wasudani na anapata matibabu hospitalini.

Ajali hiyo imejiri karibu na mji wa Omdurman.

Sheikh Noreen Muhammad Sidiq alikuwa qarii aliyepata umahushuri kutokana na usomaji wake wa Qurani wenye hisia na mvuto. Alikuwa imamu wa misikiti kadhaa katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum.

Aidha aliwahi kushiriki katika mashindano mengi ya Qur'ani katika uga wa kimataifa ikiwa ni pamoja na mashindano ya Dubai na Malaysia ambapo alipata zawadi. Mwenyezi Mungu awarehemu wote waliofariki katika ajali hiyo

Klipu ya Sheikh Noreen Muhammad Sidiq akisoma Qur'ani hii hapa chini.

3933601  

 

captcha