IQNA – Sheikh Chems-Eddine Hafiz, mlezi wa Msikiti Mkuu wa Paris, amesema mwaka 2025 ulikuwa miongoni mwa miaka migumu zaidi kwa Waislamu nchini Ufaransa, ukitawaliwa na matukio ya vurugu yaliyofikia kiwango cha “kuuawa kwa misingi ya dini.”
IQNA – Katibu Mkuu wa Hizbullah amemkumbuka Shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani kwa kusifu nafasi yake ya kipekee katika kupinga Marekani, akieleza kuwa kazi yake ilikuwa kiini cha Mhimili wa Muqawama (Mapambano).
IQNA – Naibu mkurugenzi wa kitamaduni wa Msikiti wa Jamkaran mjini Qom, Iran, amesema zaidi ya watu 16,000 wamesajiliwa kushiriki katika ibada ya Itikafu ya mwezi wa Rajab.
IQNA – Harakati ya mapambano ya Kiislamu ya Lebanon, Hizbullah, imelaani uvamizi wa Marekani dhidi ya Venezuela na mashambulizi ya miundombinu muhimu, maeneo ya kiraia na makazi katika taifa hilo la Amerika ya Kusini.
IQNA – Sheikh Ahmed Ahmed Nuaina, qari mashuhuri kutoka Misri, alisoma Qur’an katika msikiti wa Milwaukee, jimbo la Wisconsin, Marekani, Jumamosi jioni.
IQNA-Wanaharakati wa kutetea haki za Wapalestina wamemsifu Meya wa Jiji la New York, Zohran Mamdani, kwa kufuta amri za kiutawala zilizokuwa zikizuia shughuli za makundi yanayounga mkono Palestina.
IQNA – Harakati ya Ansarullah ya Yemen imetoa tamko kali kulaani shambulio la kijeshi lililofanywa na Marekani dhidi ya Venezuela, ikilitaja kuwa kitendo cha jinai.
IQNA – Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kwamba kwa kumtegemea Mwenyezi Mungu na kusimama pamoja na wananchi “Inshaallah, tutampigisha magoti adui.”
IQNA – Imam Ali (AS) si mfano tu wa uchaji Mungu kama mtu binafsi na usafi wa moyo, bali pia ni kielelezo adimu cha uongozi wa haki, uwajibikaji na unaomweka mwanadamu katikati ya utawala, afisa mmoja wa Iraq amesema.
IQNA-Kampeni ya ‘Nadhiri ya Itikafu’, ambapo watu wanachangia kugharamia ibada ya Itikafu misikitini imezinduliwa nchini Iran. Itikafu ni kujitenga kwa ajili ya ibada, na nadhiri ni ahadi ya kidini na jukumu la hiari.
IQNA-Qari kutoka Iran ameshiriki katika usomaji Qur’an Tukufu katika hafla maalum iliyofanyika mjini Kakani, Bosnia na Herzegovina, usiku wa kuamkia Mwaka Mpya.
Amri ya hivi karibuni ya utawala wa Israel, iliyondoa mamlaka ya manispaa ya al-Khalil (Hebron) katika maamuzi ya mipango kuhusu eneo nyeti la msikiti huo, inaendelea kukosolewa vikali.
IQNA- Jamii ya Kiislamu Afrika Mashariki na hasa nchini Tanzania imekumbwa na msiba mkubwa kufuatia kufariki dunia kwa mwanazuoni mashuhuri, na mfasiri wa Qur'ani Tukufu, Sheikh Ali Jumaa Mayunga, aliyefariki dunia tarehe 1 Januari 2026, jijini Dar es Salaam, Tanzania.
IQNA-Rais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia amezinukuu ripoti za kiitelijinsia na kusema kuwa eneo lililojitenga la na nchi hiyo la Somaliland limekubali kuwapokea Wapalestina na kuanzishwa kambi ya kijeshi ya Israel katika eneo hilo mkabala wa kutambuliwa rasmi na Israel.