IQNA

Waislamu Uingereza

Waislamu Uingereza ni wakarimu, huchanga Pauni bilioni moja za misaada kila mwaka

20:02 - March 01, 2023
Habari ID: 3476643
TEHRAN (IQNA) – Waislamu wa Uingereza wanaripotiwa kutoa kiasi cha pauni bilioni 1 kwa mashirika ya misaada kila mwaka jambo linaloashiria uzingatiaji wao wa mafundisho ya Kiislamu kuhusu ukarimu.

TEHRAN (IQNA) – Waislamu wa Uingereza wanaripotiwa kutoa kiasi cha pauni bilioni 1 kwa mashirika ya misaada kila mwaka jambo linaloashiria uzingatiaji wao wa mafundisho ya Kiislamu kuhusu ukarimu.

Taasisi ya Ayaan Institute yenye makao yake mjini London imethibitisha kwamba Waislamu wa Uingereza ni miongoni mwa makundi ya kidini yenye ukarimu zaidi nchini humo, na kufichua kwamba wanatoa angalau pauni bilioni moja kwa mwaka kwa ajili ya kuwasaidia wasiojiweza.

Kiwango hicho kinatarajiwa kufikia £4bn ifikapo 2050, ilifichuliwa katika ripoti iliyopewa jina, "Kusaidia Ummah: Kuchambua Sekta ya Usaidizi ya Kibinadamu ya Kiislamu nchini Uingereza."

"Sekta ya hisani ya Waislamu inatoa mchango muhimu kwa jamii ya Uingereza, uchumi, jamii ya Waislamu na inasaidia watu kote ulimwenguni. Utoaji misaada hii una chimbuko katika  imani ya Kiislamu na jambo linalostahili kutambuliwa zaidi,” Jahangir Mohammed, Mkurugenzi wa Taasisi ya Ayaan, alisema.

Taasisi ya Ayaan ni taasisi huru ya wasomi yenye makao yake London, Uingereza. Katika Uislamu, Zaka na Khums ni fedha au bidhaa ambazo ni wajibu kwa Waislamu wenye uwezo kutoa kwa ajili ya kuwasaidia  masikini

Mwenyezi Mungu anasema katika Qur'ani Tukufu Sura ya 2 Surah Baqarah aya ya 274:

Wale wanao toa mali zao usiku na mchana, kwa siri na dhaahiri, wana ujira wao kwa Mola wao Mlezi; wala haitakuwa khofu juu yao, wala hawatahuzunika. 

3482653

captcha