IQNA

Khums katika Uislamu /7

Vishawishi vya shetani vya kuepuka kulipa Khums

10:53 - November 23, 2023
Habari ID: 3477932
TEHRAN (IQNA) - Wakati mwingine, kutokana na vishawishi vya shetani, mtu anaweza kufikiri amefanya mema mengi na kuwasaidia maskini na, kwa hiyo, hana haja ya kutoa Khums.

Hii ni kwa sababu mtu anapoamua kulipa kile anachotakiwa kulipa kidini, kama vile Khums, Shetani humuonya kuhusu kutumbukia katika umasikini akifanya hivyo. “ Shet'ani anakutieni khofu ya ufakiri na anakuamrisheni mambo machafu. Na Mwenyezi Mungu anakuahidini msamaha na fadhila zitokazo kwake. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa, Mwenye kujua.” (Aya ya 268 ya Surah Al-Baqarah)

Lakini Mwenyezi Mungu anaapa katika Qur'ani Tukufu kwamba ataifidia:

“Sema: Kwa hakika Mola wangu Mlezi humkunjulia riziki na humdhikisha amtakaye katika waja wake. Na chochote mtakacho kitoa Yeye atakilipa. Naye ni Mbora wa wanao ruzuku.” (Aya ya 39 ya Surah Saba)

 Na shikeni Sala na toeni Zaka; na kheri mtakazo jitangulizia nafsi zenu mtazikuta kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu anayaona mnayo yafanya..” (Aya ya 110 ya Surat Al-Baqarah

“Watoto na mali ni pambo la maisha ya dunia, lakini kwa matendo yanayoendelea kuzalisha wema mtu anaweza kupata malipo bora kutoka kwa Mwenyezi Mungu na kuwa na matumaini makubwa Kwake.” (Aya ya 46 ya Surah Al-Kahf)

"  Mali na wana ni pambo la maisha ya dunia. Na mema yanayo bakia ni bora mbele ya Mola wako Mlezi kwa malipo, na bora kwa matumaini." (Aya ya 96 ya Surah An-Nahl)

“Mfano wa wanao tumia mali zao katika Njia ya Mwenyezi Mungu ni kama mfano wa punje moja iliyo chipuza mashuke saba. Katika kila shuke zimo punje mia. Na Mwenyezi Mungu humzidishia amtakaye, na Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa na Mwenye kujua." (Aya ya 261 ya Surah Al-Baqarah)

Iwapo Shetani atashindwa kumsadikisha mtu kukwepa kulipa Khums, atajaribu kumshawishi kuiahirisha, akisema: Naam, ndiyo, kulipa Khums ni Wajib (wajibu), lakini huna haja ya kufanya haraka. Namna gani ikiwa unakabiliwa na tatizo la kifedha? Je, ikiwa utapata hasara? Je kama…?

Qur'ani Tukufu inaonya dhidi ya ucheleweshaji kama huo:

  1. Katika Qur'ani Tukufu neno "Baghtatan" (kifo cha ghafla) limetumika katika Aya nyingi, huku likitahadharisha kuwa kifo cha ghafla kinaweza kukujia hivyo utapoteza fursa ya kufanya wema na kutekeleza wajibu wako.
  2. Qur'ani Tukufu inataja kisa cha watu binafsi na watu wanaokabiliwa na adhabu ya Mwenyezi Mungu kwa ghafla.
  3. Qur'ani Tukufu inawazungumzia baadhi ya watu wa Akhera ambao wanatamani wangerejea duniani wafanye matendo mema lakini hilo halitatokea kamwe.
  4. Katika Aya ya 14 ya Sura Al-Hadid, Quran inaashiria mjadala baina ya wakaao motoni na watu wa peponi: “Watawaita wawaambie: Kwani vile hatukuwa pamoja nanyi? Watawaambia: Ndiyo, lakini mlijifitini wenyewe, na mkasitasita, na mkatia shaka, na matamanio ya nafsi zenu yakakudanganyeni. mpaka ilipo kuja amri ya Mwenyezi Mungu, na mdanganyifu akakudanganyeni msimfuate Mwenyezi Mungu.”
Kishikizo: khums
captcha