IQNA

Khums katika Uislamu /6

Khums wakati wa Uhai wa Mtume Muhammad (SAW)

16:03 - November 15, 2023
Habari ID: 3477897
TEHRAN (IQNA) – Kupokea Khums kulikua jambo la kawaida katika zama za Mtukufu Mtume SAW).
  1. Katika Aya za Qur'ani Tukufu na Hadithi, Zakat imetajwa zaidi kuliko Khums. Labda ni kwa sababu, isipokuwa wachache huko Makka na katika makabila fulani waliokuwa wafanyabiashara, watu wengi waliishi kwa kulima na kufuga mifugo. Hata hivyo, Mtukufu Mtume (SAW) alikuwa akiwatuma baadhi ya watu katika maeneo mbalimbali kukusanya Khums. Kwa mfano, imeandikwa katika historia kwamba Mtume (SAW) alimtuma Ali bin Abi Talib (AS), Amr bin Hazm na Muadh ibn Jabal kwenda Yemen na Muhammiya kwa kabila la Bani Zayd kukusanya Khums.
  2. Akiwahutubia wajumbe waliokuja kumuona, Mtukufu Mtume (SAW) aliashiria (haja ya kulipa) Khums pamoja na kuzungumzia Sala na Zaka.
  3. Mtukufu Mtume (SAW) aliitaja Khums katika barua alizotuma kwa makabila.
  4. Pamoja na kupeleka Zakat, Waislamu walipeleka Khums kwa Mtukufu Mtume (SAW).
Kishikizo: khums
captcha