IQNA

Zaka katika Uislamu /8

Madhara ya kutolipa Zaka

18:39 - December 17, 2023
Habari ID: 3478049
IQNA – Kukataa kutoa Zaka kwa mwenye uwezo ni dhambi kwani maana yake ni kuacha Wajib (kitendo cha faradhi) katika dini tukufu ya Kiislamu. Pia kutotoa Zaka huwa matokeo mabaya ya kibinafsi na kijamii.

Haya hapa ni baadhi ya matokeo ya kutotoa Zaka.

Kupoteza mali ya mtu

Imam Sadiq (AS) alisema hakuna mali au utajiri unaopotea baharini au nchi kavu  isipokuwa kwa kushindwa kutoa Zaka ya mali au utajiri.

Imam Sadiq (AS) pia alisema: “Weka bima ya mali yako kwa kutoa Zaka na ikiwa baada ya kutoa Zaka utapoteza sehemu ya mali yako nitakudhamini (marejesho yake).”

Hasara mara mbili

Kwa mujibu wa Hadithi, ikiwa mtu atashindwa kulipa Zaka na asitumie pesa zake kwenye njia iliyo sawa, atatumia mara mbili zaidi utajiri wake katika njia ya uwong, yaani isiyo na faida.

Matumizi kwenye njia ya wahalifu

Mtukufu Mtume (SAW) alisema mtu ambaye anakataa kwa hiari kutumia pesa zake kwenye njia ya watu wema atalazimika kuzitumia kwenye njia ya waovu kwa kusitasita.

Kunyimwa fursa ya kutengeneza maeneo ya kidini

Qur’ani Tukufu inasema: “Hakika wanao amirisha misikiti ya Mwenyezi Mungu ni wale wanao muamini Mwenyezi Mungu, na Siku ya Mwisho, na wakashika Sala, na wakatoa Zaka, na wala hawamchi ila Mwenyezi Mungu. Basi huenda hao wakawa katika waongofu.” (Aya ya 18 ya Surah At-Tawbah)

Kupoteza baraka za dunia

Mtukufu Mtume (SAW) alisema kwamba Zakat isipotolewa, ardhi itazuia baraka zake kuwafikia watu.

Pia, Imam Baqir (AS) alisema kama Zaka haitalipwa, baraka zitaondolewa kwenye kilimo, matunda na migodi.

Ishara ya Nifaq (unafiki)

Aya ya 67 ya Surah At-Tawbah inaeleza sifa za mnafiki:

 Wanaume wanaafiki na wanawake wanaafiki, wote ni hali moja. Huamrisha maovu na huyakataza mema, na huifumba mikono yao. Wamemsahau Mwenyezi Mungu, basi na Yeye pia amewasahau. Hakika wanaafiki ndio wapotofu."

Kukataliwa kwa maombi na matendo mengine ya ibada

Kwa mujibu wa Hadithi, vitendo vyote (vitendo vya ibada) vinakubaliwa (na Mwenyezi Mungu) ikiwa Sala ya mtu itakubaliwa, na Sala ya mtu inakubaliwa ikiwa atatoa Zaka.

Imamu Ridha (AS) amesema Mwenyezi Mungu ameweka pamoja Salah na Zaka na haitakubaliwa Salah bila ya Zaka.

Nabii Musa (AS) alimuona kijana mmoja akisali kisha akasema anasali kwa uzuri. Hapo aliambiwa na Mwenyezi Mungu kwamba Sala ya kijana huyo haikubaliwi kwa sababu yeye ni bakhili na halipi Zaka.

Kuwa sawa na mtoa riba

Imamu Ali (AS) alisema mtu anayekataa kutoa Zaka ni sawa na mtoaji riba.

Kukataa kutoa Zaka pia ni sawa na wizi. Kwa mujibu wa Hadithi, kuna aina tatu za wezi, mmoja wao akiwa ni mtu asiyetoa Zaka.

Kishikizo: Zaka
captcha