IQNA

Waislamu Uingereza

Polisi wa Uingereza Watuhumiwa Kuwatendea Waislamu waliozuiliwa kama Magaidi

20:57 - December 09, 2022
Habari ID: 3476220
TEHRAN (IQNA) – Waislamu kadhaa wa Uingereza wamewashutumu polisi wa nchi hiyo kwa kuwatendea vibaya kama "magaidi" wakati walipokamatwa kwa tuhuma za chuki dhidi ya Wayahudi ambazo baadaye zilitupiliwa mbali.

Adil Mota, Mohammed Hanif, Asif Ali na Jawad Hussain walishtakiwa kwa kupiga kelele dhidi ya Wayahudi mnamo Mei 2021 waliposafiri kutoka Blackburn kuunga mkono maandamano ya kuunga mkono Palestina. Wakati huo, Israel ilikuwa ikishambulia kwa mabomu Gaza na mamia ya Wapalestina waliuawa katika shambulio hilo la kinyama, na kusababisha maandamano makubwa katika miji mikuu ya nchi za Ulaya yakiwemo maandamano makubwa mjini London.

Waislamu hao wanne wa Uingereza wa Blackburn walishtakiwa kwa kutumia maneno ya kutisha, matusi kwa nia, ambayo huenda ilichochea chuki dhidi ya Wayahudi. Walikamatwa kutokana na video iliyosambaa mtandaoni ambayo ilionyesha magari yakiwa na bendera za Palestina yakipita katika jamii ya Wayahudi kaskazini mwa London huku washiriki wakipiga kelele za chuki dhidi ya Wayahudi.

Kesi ya wanne hao iliendelea kwa takriban miezi 18 lakini mwezi uliopita mashtaka yaliondolewa baada ya mwendesha mashtaka kutangaza hakuna matarajio ya kweli ya kufaulu.

Wakizungumza kwa mara ya kwanza, washtakiwa watatu wameeleza jinsi maisha yao yalivyopinduliwa na tukio hilo la kutisha. Wakiandamana na wakili wao, Ghaffar Khan, watatu hao walisema kuwa polisi waliwatendea vibaya na hawakujali haki zao wakati wa kuwakamata na kuendelea.

Wote walisema kuwa magari ya polisi yaliyokuwa yamewabeba askari wa kupambana na ugaidi yalisalia yameegeshwa nje ya nyumba zao kwa karibu miezi miwili, na kusababisha aibu na fedheha kwao katika jamii ya eneo hilo. Walisema kuwa polisi walivamia nyumba zao na kuchukua mali ambazo hazijarejeshwa hadi sasa, hata baada ya kufutwa kwa mashtaka.

3481593

captcha