IQNA

Khums katika Uislamu /8

Jinsi Khums na Zaka zinavyotofautiana na Ushuru

15:18 - November 29, 2023
Habari ID: 3477963
TEHRAN (IQNA) - Khums na Zaka ni pesa au mali zinazopokelewa na taasisi za kidini za Kiislamu wakati ushuru unakusanywa na serikali.

Je, ni vipi hasa Khums na Zaka zinatofautiana na kodi? Hapa kuna baadhi ya tofauti:

Ushuru ni pesa unazolipa ili serikali ikupe huduma kama vile kujenga barabara, kujenga bustani na kutoa huduma kama vile za afya na usalama.

Tofauti ya pili ni kwamba kulipa Khums na Zaka ni ibada inayohitaji Nia ya Qurba (nia ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu) lakini hakuna jambo kama hilo katika kulipa kodi, jambo ambalo kwa kawaida hufanywa upende usipende, yaani ni lazima kwa mujibu wa sheria za nchi na wasiofanya hivyo huadhibiwa kwa kutozwa faini, kufungwa jela, n.k

Tofauti ya tatu ni kwamba Khums inatumika chini ya uangalizi wa mwanachuoni msomi zaidi, mchamungu, na maarufu, ambapo kodi zinaweza zisitumike kwa njia ya haki na uadilifu.

Tofauti ya nne ni kwamba Khums na Zaka hulipwa kwa kuzingatia uaminifu. Kwanza mtu mwenyewe, si mwajiriwa wa serikali, anahesabu mapato yake na gharama kwa ajili ya kuamua ni kiasi gani anachopaswa kulipa kama Khums na Zakat. Pili, anaweza kuchagua Marjaa Taqlid ambaye anataka kumpa Khums au Zaka yake. Tatu, anajua jinsi inavyotumika chini ya usimamizi wa mwanachuoni msomi na mwadilifu.

Tofauti ya tano ni kuwa mpokeaji wa Khums na Zakat anaipokea kwa lengo la kuwasaidia watu kukua na kutakasa mali zao na mwenye kutoa Khums na Zaka anafanya hivyo kwa lengo la kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu.

Pia, Khums huhesabiwa kulingana na kile kinachosalia kutoka kwa gharama za mtu kwa mwaka wakati ushuru huhesabiwa kulingana na mapato ya mtu.

Kishikizo: khums Zaka
captcha