IQNA

Ujumbe

Rais wa Iran: Wanaodai kuwa wafuasi wa Nabii Isa (AS) hawapaswi kuiunga mkono Israel

20:35 - December 25, 2023
Habari ID: 3478091
IQNA-Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, kuwa, wale wote wanaodai kwamba ni wafuasi wa Nabii Issa Masih (as) hawapaswi kuiunga mkono Israel na mauaji yake dhidi ya watoto huko katika Ukanda wa Gaza.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, mwanzoni mwa mwaka mpya, Wakristo wote na mataifa yote na dhamiri zote za dunia zinapaswa kupaza sauti zao za kuchukizwa na ukatili na jinai na mauaji ya halaiki katika Ukanda wa Gaza na zitake kusitishwa mauaji hayo ya kutisha dhidi ya watu wanaodhulumiwa wa eneo hilo.

Seyyed Ebrahim Raisi sambamba na kutoa pongezi za maadhimisho ya kumbukumbu ya kuzaliwa Nabii Isa Masih (as) kwa Wakristo wa Iran na  wote wanaotaka haki amesema kuwa, kutekelezwa uadilifu na kupambana na dhulma ni miongoni mwa yaliyokuwa mafundisho ya Mtume huyo mkubwa wa Mwenyezi Mungu na kuongeza kuwa: "Leo hii baadhi ya nchi zinazodai kumfuata Nabii Issa zinauunga mkono utawala haramu wa Israel katika dhulma, jinai, mauaji dhidi ya watoto na uporaji wa haki za Wapalestina unaofanya na utawala huo dhalimu katika hali ambayo Nabii Issa alikuwa mlinganiaji wa uadilifu na vita dhidi ya dhulma.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran aidha amesema: Kwa uungaji mkono wa baadhi ya nchi za Magharibi, Waislamu, Wakristo, misikiti na makanisa ya Ukanda wa Gaza yamehujumiwa na Israel mtenda jinai.

Siku kama ya leo miaka 2023 iliyopita, kwa mujibu wa baadhi ya riwaya, Nabii Isa Masih (AS) alizaliwa katika mji wa Bait Laham (Bethlehem) huko Palestina.

Inafaa kuashiria hapa kwamba, siku ya leo ya tarehe 25 Disemba kila mwaka inajulikana kote duniani hasa kwa Wakristo kuwa ni siku ya Sikukuu ya Krismasi.

captcha