IQNA

Maelewano ya kidini

Msikiti nchini Pakistan wafungua milango kwa wauminiWakristo

22:59 - August 21, 2023
Habari ID: 3477474
ISLAMABAD (IQNA) - Msikiti katika mji wa Jaranwala, mkoa wa Punjab wa Pakistan, ulifungua mlango wake kwa Wakristo wanaohitaji mahali pa ibada.

Mchungaji aliviambia vyombo vya habari vya kimataifa kwamba msikiti mmoja huko Jaranwala umefungua milango ya majengo yake kwa jumuiya ya Wakristo kwa ajili ya ibada zao.
Alisema afisa wa utawala wa msikiti huo alimwendea na akamkaribisha msikitini kwa ajili ya ibada kama wanavyofanya kanisani.
Ilikuja baada ya makanisa ya Wakristo kuharibiwa na kuchomwa moto huko Jaranwala eneo la Faisalabad kwa madai ya kukufuru.
Mapema mwezi huu, makanisa matano na majengo kadhaa yameteketezwa na makazi ya waumini wa Kikristo, waliokuwa wakituhumiwa kwa kufuru, kuharibiwa.
Mchungaji wa eneo hilo aliambia vyombo vya habari kwamba makanisha ya Salvation Army, Shehroonwala Church, United Presbyterian Church, Allied Foundation Church yamevamia makundi ya watu.
Kaimu Waziri Mkuu wa Pakistan Anwaarul Haq Kakara amekosoa uvamizi huo na akataja siku ya tukio hilo kuwaa siku ya aibu. Katika chapisho kwenye mtandao wa kijamii aliapa kuwaadhibu wale waliohusika na kudharau makanisa kwa madai ya Kukufuru.
Alisema, "Nimechoshwa na taswira zinazotoka Jaranwala, Faisalabad. Hatua kali zintachukuliwa dhidi ya wale wanaokiuka sheria na kulenga watu wachache. Watekelezaji sheria wote wametakiwa kuwakamata wahalifu na kuwafikisha mahakamani. Uwe na uhakika kwamba serikali ya Pakistan inasimama na raia wetu kwa usawa."
Polisi wamewakamata zaidi ya watu 150 katika kesi hiyo huku uchunguzi wa ngazi ya juu ukianzishwa kuhusiana na kisa hicho huku serikali ya Punjab ikiona kama jaribio lililopangwa la kuvuruga amani nchini humo.
.

Habari zinazohusiana
Kishikizo: pakistan wakristo
captcha