IQNA

Watetezi wa Qur'ani Tukufu

Russia yataka Tamko la Umoja wa Mataifa Kulaani vitendo vya kuvunjia heshima Qur'ani Tukufu

13:39 - December 07, 2023
Habari ID: 3478001
MOSCOW (IQNA)- Russia imetangaza kwamba inajitahidi kuandaa taarifa ya kimataifa katika Umoja wa Mataifa ya kulaani vitendo vyote kudhalilishwa au kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu na Uislamu, mwanadiplomasia wa nchi hiyo amesema.

Mwakilishi wa Kudumu wa Russia katika Mashirika ya Kimataifa huko Vienna Mikhail Ulyanov aliandika katika chapisho katika kituo chake cha Telegram kwamba nchi yake inajitahidi kuandaa taarifa kama hiyo katika Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Vienna (UNOV) ya kupinga vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu na hatua zozote zilizo dhidi ya Uislamu kama vile kuvunjia heshima Qur'ani Tukufu.

Alisema kauli hiyo itajadiliwa katika mkutano wa Tume ya Umoja wa Mataifa ya Kuzuia Uhalifu na Haki ya Jinai, unaotarajiwa kufanyika Ijumaa hii Desemba 8.

Huko nyuma mwezi wa Juni, Rais wa Russia Vladimir Putin alisema kuvunjia heshima Qur'ani Tukufu hakuonekani kama uhalifu katika baadhi ya nchi za Magharibi lakini nchini Russia ni kinyume cha sheria na wahusika wanaadhibiwa.

Putin aliongeza kuwa: "Qur'ani  ni takatifu kwa Waislamu na inapaswa kuwa takatifu kwa wengine," alisema na kuongeza, "Siku zote tutazingatia sheria hizi."

4186254

captcha