IQNA

Msikiti mkubwa zaidi Ulaya wafunguliwa Moscow

5:22 - September 24, 2015
Habari ID: 3366927
Rais Vladmir Putin wa Russia Jumatano amefungua msikiti mkuu wa Moscow ambao ni msikiti mkubwa zaidi barani Ulaya.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, sherehe ilihudhuriwa na viongozi na wawakilishi wa nchi mbalimbali za  duniani akiwemo Rais Recep Tayyip Erdoğan wa Uturuki na Mahmoud Abbas, Rais wa  Palestina. Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Hossein Amir-Abdollahian, aliongoza ujumbe wa Iran katika ufunguzi wa msikiti huo ambao ujenzi wake umegharimu takribani dola milioni 170, sehemu kubwa ya gharama hizo ikiwa imetokana na michango ya watu binafsi. Ujenzi wa msikiti huo, ambao umefanyika kwenye eneo ulipokuwepo msikiti mdogo wa kale wa zaidi ya miaka 100, umechukua muda wa miaka 10 hadi kukamilika. Msikiti huo uliofunguliwa kwa mnasaba wa kuwadia Sikukuu ya Idul-Adh’ha una ghorofa sita na utakuwa na uwezo wa kuchukua waumini elfu kumi. Uislamu ni dini ya pili yenye wafuasi wengi zaidi nchini Russia ambao idadi yao inafika milioni 23, na akthari yao wanaishi katika jamhuri za Kaukasia ya Kaskazini. Waislamu wanaokadiriwa kufika milioni mbili wanaishi katika mji mkuu wa Russia, Moscow, ambao mbali na msikiti mkuu uliofunguliwa leo una misikiti mingine mitano tu kwa ajili ya Waislamu wa nchi hiyo…/

3366786

captcha