IQNA

Misikiti 7,500 imejengwa Russia wakati wa urais wa Putin

12:03 - December 09, 2015
Habari ID: 3461608
Mwanazuoni mwandamizi wa Kiislamu nchini Russia amesema misikiti 7,500 mipya imejengwa nchini humo wakati wa kipindi cha urais wa Vladimir Putin.

Sheikul Islam  Talgat Tajuddin amesema misikiti hiyo imejengwa na Waislamu nchini Russia.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mwanazuoni huyo amesema idadi hiyo kubwa ya misikiti kujengwa Russia ni jambo lisilo na kifani na kuongeza kwamba idadi hiyo ni kubwa ikilinganishwa na wakati wa  rais wa zamani Boris Yelstin na mtawala wa mwisho wa Shirikisho la Sovieti Mikhail Gorbachev.
Uislamu ni dini ya pili kwa wingi wa wafuaasi nchini Russia. Waislamu ni takribani ya asilimia 15 ya idadi ya wa watu wote  milioni 143 nchini humo.
Kwingineko katika matamshi yake, Sheikh Tajuddin ameleeni ugaidi wa makundi kama vile ISIS au Daesh huku akitoa wito kwa Waislamu kuungana dhidi ya makundi ya kigaidi.../

3461539

captcha