IQNA

Sura za Qur’ani Tukufu /109

Mtazamo wa Uislamu kuhusu dini mbalimbali katika Sura Al-Kafirun

22:31 - August 28, 2023
Habari ID: 3477511
TEHRAN (IQNA) – Katika aya moja ya Qur’an Mwenyezi Mungu anamwamrisha Mtume Muhammad (SAW) awaambia makafiri wabakie na dini yao.

Baadhi wanaamini kwamba aya hii, iliyo katika Sura Al-Kafirun, ni ushahidi kwamba Uislamu unahimiza maelewano ya wafuasi wa dini mbali mbali.

Al-Kafirun ni sura ya 109 ya Qur’ani Tukufu, ambayo ina aya 6 na iko katika Juzuu ya 30.

Ni Makki na Sura ya 18 iliyoteremshwa kwa Mtukufu Mtume Muhammad (SAW).

Sura inawahusu Kafirun (makafiri), na neno Kafirun limekuja katika Aya ya kwanza, na kwa hiyo jina la Sura.

Mwenyezi Mungu katika sura hii anamuamuru Mtume (SAW) abainishe upinzani wake kuhusu ibada ya masanamu na atangaze kwamba yeye hana maslahi na dini ya Kafirun na hatapatanisha nao. Mungu pia anamfahamisha kwamba makafiri hawataikubali dini yake.

Dini ya makafiri haikubaliwi na Mtume Muhammad  (SAW) wala hawakubali dini ya Mtume (SAW). Kwa hiyo, wasitarajie Mtume (SAW) kuelewana nao.

Sura hii ni ujumbe wa Mwenyezi Mungu kwa Mtume (SAW) kuwajibu makafiri.

Katika aya tatu za mwanzo Mwenyezi Mungu anamwamrisha Mtume (SAW) kumwabudu Yeye daima na kuwaambia makafiri kwamba wao kamwe hawatamwabudu Mwenyezi Mungu na hivyo hakuna maelewano kati ya Waislamu na makafiri katika masuala ya dini.

Hivi ndivyo ilivyo maadamu makafiri wanasisitiza juu ya imani yao. Hizi hapa ni aya za 1-6 Sura hii.

 “(Muhammad), Sema: Enyi makafiri! Siabudu mnacho kiabudu;  Wala nyinyi hamuabudu ninaye muabudu. Wala sitaabudu mnacho abudu. Wala nyinyi hamuabudu ninaye muabudu. Nyinyi mna dini yenu, nami nina Dini yangu.”

”Marudio haya ni msisitizo juu ya ukweli kwamba Mtume Muhammad (SAW) anapaswa kumuabudu Mwenyezi Mungu kwa hali yoyote ile.

Aya ya mwisho inatenganisha kikamilifu njia ya Waislamu na makafiri. Hapa wengine wanaweza kusema kwamba Uislamu umekubaliana na chaguo la makafiri la dini waitakayo na Mwenyezi Mungu amemhimiza Mtume (SAW) asiwapinge. Wengine pia wameifasiri aya hii kuwa ina maana ya kukubali Uislamu kuwepo dini mbali mbali.

Lakini tafsiri hizi haziwezi kuwa sahihi kwa sababu Uislamu siku zote unalenga kuwalingania watu kwenye Tauhidi na kujitenga na Kufr na Shirki.

Baadhi ya wafasiri wanaamini kwamba neno ‘Dini’ katika Aya ya mwisho lina maana ya malipo na adhabu, si dini kama kama imani tunavyifahamu. Kwa hivyo, Aya ina maana kila kundi la watu litalipwa au kuadhibiwa kwa kuzingatia njia wanayoifuata.

Habari zinazohusiana
captcha