IQNA

Mawaidha

Sura Al-Fatiha: Sura ya Kumsifu, Kumuomba Mwenyezi Mungu

15:19 - January 10, 2024
Habari ID: 3478175
IQNA - Surah Al-Fatiha ndio sura pekee ya Qur'ani Tukufu ambayo aya zake zote zinahusu kuswali na kumwabudu Mwenyezi Mungu.

Sehemu ya kwanza ya Sura inahusu kumhimidi Mwenyezi Mungu na sehemu ya pili, mahitaji ya mwenye kuabudu yametajwa.

Sura iliyoteremshwa Makka ina aya saba. Hizi ni baadhi ya sifa za Surah Al-Fatiha:

  • Ni tofauti kwa uwazi na sura zingine katika suala la sauti na mtiririko. Katika Sura hii, Mwenyezi Mungu anatufundisha jinsi ya kumuomba na kuzungumza Naye. Sura inaanza kwa kumhimidi Mwenyezi Mungu na kudhihirisha imani kwa Mwenyezi Mungu na Ufufuo. Inamalizia kwa maombi kutoka kwa Mwenyezi Mungu na kuzungumzia mahitaji ya waja wa Mungu.
  • Sura Al-Fatiha ndio msingi wa Qur'ani Tukufu. Kwa mujibu wa Hadithi, Mtume Muhammad (SAW) alimwambia mmoja wa masahaba zake, Jabir ibn Abdullah Ansari: “Je, unataka nifundishe Sura bora zaidi ambayo Mwenyezi Mungu Ameiteremsha katika kitabu Chake? Kisha Mtume (SAW) akamfundisha Surah Al-Fatiha, ambayo pia inajulikana kama Ummu al-Kitab, na akasema Sura hii ni ponyo la kila maumivu isipokuwa kifo. Umm maana yake ni mzizi na msingi. Labda ndio maana Ibn Abbas, mfasiri mashuhuri wa Qur'ani Tukufu anasema: Kila kitu kina msingi na msingi na msingi wa Quran ni Sura Al-Fatiha.
  • Katika aya za Quran, Surah Al-Fatiha imetambulishwa kama zawadi kubwa kwa Mtukufu Mtume (SAW):

(Muhammad), Tumekupa Aya saba zinazorudiwa mara kwa mara na Qur'ani Tukufu." (Aya ya 87 ya Surah Hijr)

Sura imegawanyika sehemu mbili na sehemu ya kwanza ni juu ya kumhimidi Mwenyezi Mungu na katika sehemu ya pili mahitaji ya mwenye kuabudu yametajwa.

Kwa mujibu wa Hadithi kutoka kwa Mtukufu Mtume Muhamamd (SAW), Mwenyezi Mungu amesema: “Nimeigawa Sura ya Fatiha baina Yangu na mja Wangu katika sehemu mbili, na mja Wangu atapata alichoomba.

"Ujira wa Muislamu yeyote anayesoma Surah Al-Fatiha ni kama ule wa mtu aliyesoma thuluthi mbili ya Qur'ani Tukufu, na atapata malipo mengi kama kwamba amempa kila Muislamu Muumini, mwanamume au mwanamke sadaka."

3486724

 

captcha