IQNA

Sura za Qur'ani Tukufu / 43

Sura Az-Zukhruf inaashiria mahali ambapo matukio yote yanasajiliwa

18:05 - November 29, 2022
Habari ID: 3476168
TEHRAN (IQNA) – Mwenyezi Mungu anafahamu matukio na matukio yote na wakati huo huo amewapa wanadamu uhuru wa kuchagua kubainisha hatima yake.

Kwa mujibu wa Surah Az-Zukhruf ya Qur'ani Tukufu, kuna mahali ambapo matukio yote yaliyotokea huko nyuma na yatakayotokea baadaye yanasajiliwa.

Sura ya 43 ya Quran ni Surah Az-Zukhruf. Ina Aya 89 na imo katika Juzuu ya 25. Ni Sura Makki yaani iliteremeshwa mjini Makka na  ni Sura ya 63 iliyoteremshwa kwa Mtukufu Mtume Muhammad (SAW).

Jina la Sura linatokana na neno Zukhruf, lenye maana ya mapambo, yaliyotajwa katika Aya ya 35 ambayo inaashiria  dunia ilivyo na kusema: " Na mapambo. Lakini hayo si chochote ila ni starehe ya maisha ya dunia tu, na Akhera iliyoko kwa Mola wako Mlezi ni ya wenye kumchamngu. "

Sura inazungumzia umuhimu wa Qur'ani Tukufu, utume wa Mtume Muhammad (SAW), baadhi ya sababu za Tauhidi na haja ya kukabiliana na Shirki (ushirikina).

Pia inaashiria hadithi za baadhi ya Mitume wa Mwenyezi Mungu na watu wao. Kwa mujibu wa wafafanuzi wa Quran, mada kuu ya Sura hii ni kutoa onyo kwa wanadamu.

Mwanzoni mwa sura, mkazo umewekwa juu ya umuhimu wa Quran Tukufu na utume wa Mtume wa mwisho wa Mwenyezi Mungu.

Kisha inazungumzia sababu zinazothibitisha Tauhidi na kutaja baraka za Mwenyezi Mungu.

Sura pia inasisitiza kukabiliana na Shirki na kuepuka ushirikina na uigaji upofu, ikionyesha jinsi manabii kama Ibrahim (AS), Musa (AS) na Isa (AS) walivyotenda katika suala hili.

Kisha kuna suala la kufufuliwa na jinsi waumini wanavyolipwa na ni hatima mbaya iliyoje inayowangoja makafiri.

Pia inarejelea maadili yasiyokubalika ambayo yanatawala maisha ya makafiri, na kuwaongoza kufanya makosa katika maswala muhimu maishani.

Moja ya masuala yaliyotajwa katika Sura Az-Zukhruf ni mahali panapojulikana kama Umm al-Kitab na Luh Mahfuz. Umm al-Kitab pia ametajwa katika Sura Al-Imran na Ar-Ra'ad. Kwa mujibu wa baadhi ya Hadithi, Umm al-Kitab inarejelea Qur'an Tukufu nzima wakati kwa mujibu wa baadhi ya wengine inahusu tu Surah Al-Fatihah.

Luh Mahfuz ni mahali ambapo matukio yote yanayotokea duniani yamesajiliwa kwa maelezo kamili na kwa njia ambayo haiwezi kubadilishwa.

Haijulikani kitabu hiki kimeundwa na nini, lakini kwa hakika hakijatengenezwa kwa karatasi na sio nyenzo.

 

Habari zinazohusiana
captcha