IQNA

Janga la corona

Maulamaa Pakistan wapinga kufungwa misikiti katika mwezi wa Ramadhani

12:43 - April 16, 2020
Habari ID: 3472671
TEHRAN (IQNA) – Maulamaa mashuhuri nchni Pakistan wametaka serikali iondoe marufuku ya sala za jamaa misikitni nchini humo katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Katika taarifa ya pamoja na maulamaa na viongozi wa vyama vya Kiislamu, wamesema kuwa Sala ya jamiini muhimu kwa Waislamu na hivyo haipaswi kupigwa marufuku maadamu kanuni za kiafya zitazingatiwa.

Takwa hilo limekuja huku Waziri Mkuu wa Pakistan Imran Khan akisisitiza kuwa atakutana na viongozi wa kidini na maulamaa kujadili marufuku ya Sala za jamaa. Tokea mwezi uliopita, Pakistan ilitangaza marufuku ya mijimuiko ikiwa ni pamoja na sala za Ijamaa ili kuzuia kuenea ugonjwa wa corona . Hadi kufikia Aprili 16, watu 6,505 walikuwa wameambukizwa corona nchini humo huku wengine 124 wakiwa tayari wameshapoteza maisha.

Marufuku ya Sala za jamaa imeibua hasria Pakistan ambapo Ijumaa iliyopita polisi walishambuliwa walipokuwa wakiwazuia watu kuingia msikitini katika mji wa Karachi.

Mufti Taqi Usmani, ambaye ni miongoni mwa maulamaa wanaotaka marufuku ya Sala za jamaa iondolewe amesema ili kukabiliana na corona, wataondoa mazulia na mikeka misikitini na kupulizia dawa za kuua virusi mara kwa mara. Aidha amesema dawa ya kunawa mikono itawekwa katika milango yote ya misikitini na waumini watatakiwa wasikaribiane wakati wa Sala.

Wataalamu wa afya nchini Pakistan wanasema Sala za jamaa ni eneo linaloweza kueneza ugonjwa hatari wa corona na kwamba mfumo wa afya nchini humo hauna uwezo wa kukabiliana na wimbi kubwa la wagonjwa.

3891980

Kishikizo: pakistan Corona sala
captcha