Kwa mujibu wa taarifa, wakaazi wa kijiji kimoja mkoani Al Minya ambao ni Waislamu na Wakristo wote wameweka kazi zao kando na kushiriki katika ukarabati wa Msikiti wa Al-Amrawiambao ulijengwa karne kadhaa zilizopita.
Inadokezwa kuwa mkaazi mmoja wa kijiji hiyo ambaye ni Mkristo ndiye aliyetoa pendekezo la kwanza kukarabatiwa msikiti huo, na baada ya wakaazi wote wa kijiji kuafiki ukarabati ulianza.
Misri ni nchi ya Kiislamu iliyo kaskazini mwa Afrika na idadi ya watu nchini humo inakadiriwa kuwa ni milioni 100. Zaidi ya asilimia 90 ya wakazi wa Misri ni Waislamu na waliosalia ni Wakristo. Watu wa Misri, wawe ni Waislamu au Wakristo wamekuwa wakiishi kwa amani na maelewano na husaidiana mara kwa mara katika masuala ya kidini.