IQNA

Waislamu Uingereza

Siku ya Tafrika katika Msikiti yapangwa huko Blackburn

16:48 - July 18, 2023
Habari ID: 3477301
LONDON (IQNA) – Masjid E Saliheen, msikiti wa Blackburn, utaandaa siku ya tafrija na kufurahisha familia wikendi hii ili kusaidia kuchangisha fedha za kuboresha vifaa vya mazishi.

Masjid E Saliheen, ambayo iko mbali na Mtaa wa Disbury, inatarajia kutoa vifaa hivyo kwa jamii kutumia bila gharama yoyote.

Msikiti huo ulisema tayari umechangisha pauni 56,000 kwa ajili ya mradi huo ambao ulisaidia kurekebisha paa linalovuja pamoja na kujenga chumba maalumu cha kutayarisha maiti kwa ajili ya maziko.

Msemaji wa msikiti alisema: "Katika jitihada za kuongeza fedha zilizobaki za kulipia vifaa na kazi, msikiti utakuwa mwenyeji wa siku yake ya tatu ya kila mwaka ya kufurahisha familia inayoitwa 'Jiko la Kimataifa la Saliheen."

Tukio hilo litafanyika Jumapili kuanzia saa tano mchana hadi sa 12 jioni katika viwanja vya msikiti.

Vibanda mbalimbali vitatoa vyakula kutoka duniani kote ikiwa ni pamoja na India, Pakistan, Tanzania, Afrika Kusini, Morocco na China.

Msemaji wa msikiti huo aliongeza hafla hiyo pia itajumuisha shughuli za bure za watoto: "Watoto pia wataweza kupakwa rangi za uso, kupamba keki zao na donati na kushiriki katika shughuli za michezo bila malipo."

3484379

captcha