IQNA

Mwezi wa Ramadhani

Mazulia yabadilishwa katika Msikiti wa Mtume (SAW) kabla ya Ramadhani

18:08 - March 06, 2024
Habari ID: 3478460
IQNA - Mazulia katika Al-Rawdah Al-Sharifa katika Msikiti wa Mtume (Al-Masjid an-Nabawi) huko Madina yamebadilishwa kwa ajili ya maandalizi ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Mamlaka ya Masuala ya Msikiti Mkuu wa Makka na Msikiti wa Mtume imetekeleza jukumu hilo la  kubadilisha mazulia.

Mazulia hayo mapya yenye ubora wa hali ya juu ni sehemu ya mfululizo wa maboresho ya huduma zinazotekelezwa na mamlaka hiyo ili kuwahudumia vyema wageni wanaotembelea msikiti huo.

Ramadhani, mwezi wa tisa katika kalenda ya Kiislamu, ni wakati unaoshuhudia ongezeko kubwa la wageni wanaotembelea msikiti huo kutoka sehemu mbalimbali za dunia.

Aidha mamlaka hiyo imetoa mafunzo kwa wanawake wa kujitolea 1,350 ili kuwapa ujuzi unaohitajika ili kutoa huduma za hali ya juu kwa wanawake wanaotembelea msikiti huo.

Mada zilizojadiliwa wakati wa mafunzo zilijumuisha usimamizi wa umati, mawasiliano na wageni kwenye misikiti, usimamizi wa hafla za kujitolea, na kuwasaidia wazee na watu wenye ulemavu.

3487447

Habari zinazohusiana
captcha