IQNA

Umrah 1445

Zaidi ya waumini milioni sita walitembelea Msikiti wa Mtume (SAW) wiki Iliyopita

21:38 - November 17, 2023
Habari ID: 3477902
MEDINA (IQNA) - Msikiti wa Mtume (SAW), Al Masjid An Nabawi, eneo la pili kwa utakatifu katika Uislamu, ulishuhudia wimbi kubwa la waumini wiki iliyopita, shirika la serikali liliripoti.

Msikiti huo uliopo katika mji wa Madina nchini Saudia ulipokea zaidi ya Waislamu milioni 6 waliosali na kuzuru kaburi la Mtume Muhammad (SAW).

Kwa mujibu wa Shirika la Urais wa Msikiti wa Mtume, idadi ya waumini ilifikia milioni 6.3 katika wiki kutoka tarehe 22 hadi 29 ya Rabi Al Akhar, mwezi wa nne wa kalenda ya mwezi wa Kiislamu. Miongoni mwao, waumini 127,671 walisali katika Al Rawda Al Sharifa, eneo ambalo kaburi la Mtume lipo.

Shirika hilo lilisema kuwa wageni wanaotembelea Al Rawda Al Sharifa wanapaswa kuweka miadi yao mapema na kuzingatia muda uliowekwa.

Mahujaji wengi wanaotekeleza Hija Ndogo ya Umra,  katika Msikiti Mkuu wa Makka, eneo takatifu zaidi katika Uislamu, pia hutembelea Msikiti wa Mtume kuswali na kutoa heshima zao kwa Mtukufu Mtume Muhammad (SAW). Saudi Arabia inatarajia takriban Waislamu milioni 10 wa kigeni kufanya Umrah wakati wa msimu huu.

Msimu wa Umrah ulianza tena zaidi ya miezi minne iliyopita baada ya Hija ya kila mwaka, ambayo ilihudhuriwa na Waislamu wapatao milioni 1.8 kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka mitatu kufuatia janga la COVID-19.

Umrah ni ibada ya hiari ambayo Waislamu wanaweza kufanya wakati wowote wa mwaka. Tofauti na Hija, ambayo ni faradhi kwa kila Muislamu mwenye uwezo na uwezo wa kifedha mara moja katika maisha, Umrah si faradhi.

3486051.

captcha