IQNA

Shakhsia katika Qur'ani Tukufu /48

Kinachowangoja wanaopinga dini

22:16 - September 20, 2023
Habari ID: 3477626
TEHRAN (IQNA) – Katika historia, kumekuwa na makundi mbalimbali ya watu wanaopinga mitume wa kiungu na mafundisho yao.

Qur'ani Tukufu inawataja baadhi ya makundi haya na watu binafsi na hatima yao.

Mtume Muhammad (SAW) alikuwa na maadui wengi akiwa kama mjumbe wa Mwenyezi Mungu. Qur'ani Tukufu inawataja baadhi yao lakini inataja moja tu. Alikuwa na uhasama wa kiwango cha juu sana ana dhidi ya Mtume (SAW) na, pamoja na mke wake, walitumia kila fursa kukabiliana na Mtume (SAW).

Surah Al-Masad iliteremshwa kuhusu mtu huyu na mke wake na matokeo ya uadui na Uislamu:

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu.

Imeangamia mikono ya Abu Lahab, na yeye pia ameangamia.  Hayatamfaa mali yake, wala alivyo vichuma. Atauingia Moto wenye mwako.  Na mkewe, mchukuzi wa kuni,  Shingoni mwake iko kamba iliyo sokotwa.

 Mtu anayeitwa Abu Lahab katika Sura hii ni Abdul Uzza bin Abdal Muttalib, ami yake Mtume (SAW). Yeye na mkewe, Umm Jamil, walimsumbua na kumvuruga sana Mtukufu Mtume (SAW) na wakafanya majaribio mengi ya kuupinga Uislamu. Aliyachukulia maneno na miujiza ya Mtume (SAW) kuwa ni uchawi na akajaribu kuzuia kuenea kwa dini.

Kwa mujibu wa Surah Al-Masad, Abu Lahab alikuwa tajiri. Muhammad (SAW) alipokuwa na umri wa miaka 8, Abdal Muttalib aliugua. Aliwakusanya wanawe ili kumwomba mmoja wao amtunze mtoto. Abu Lahab alijitolea, lakini Abdal Muttalib hakukubali.

Wakati Muhammad (SAW) alipotangaza kwamba ameagizwa na Mwenyezi Mungu kueneza ujumbe wa Uislamu kwa uwazi, Abu Lahab alianza uadui wake naye. Yeye na mkewe walikuwa wakimfuata Mtume (SAW), wakimpiga mawe na kutupa miiba na takataka katika njia yake.

Pia walikuwa wakizungumza na mtu yeyote ambaye alikubali wito wa Mtume (SAW), na kujaribu kumshawishi aachane na Uislamu.

Abu Lahab alikufa kwa ugonjwa ambao husababisha majeraha kwenye mwili. Watu wasingemwendea wakihofia kwamba wangeugua pia. Baada ya mwili wake kuanza kuoza, watu waliutoa nje ya Makka na kuurushia mawe hadi ukafunikwa na mawe.

Katika Surah Al-Masad, mke wake, Umm Jamil anarejelewa kama mtu aliyebebeshwa kuni (za kuzimu), ambayo wafasiri wa Qur'ani Tukufu wanasema inaashiria matendo yake ya kusengenya na kusimulia ambayo yatasababisha moto wa Jahannam kuenea kwa ajili yake.

captcha