IQNA

Sura za Qur'ani Tukufu / 78

‘Habari Kuu’ katika Surah An-Naba

16:00 - May 20, 2023
Habari ID: 3477021
TEHRAN (IQNA)-Watu wana shauku kubwa ya kutaka kujua mustakabali wao, wakati ujao unaowangoja katika siku na miaka ijayo na unaowangoja katika maisha ya baadaye.

Wakati ujao haujulikani lakini kuna habari muhimu sana na kuu kwa wanadamu ambazo Surah An-Naba inazungumzia. An-Naba ni jina la sura ya 78 ya Qur'ani Tukufu yenye aya 40 na ni Sura ya kwanza katika Juzuu ya 30 na ya mwisho. Ni  Sura Makki na pia ni sura ya 80 iliyoteremshwa kwa Mtukufu Mtume (SAW).

Naba maana yake ni habari na aya ya pili inazungumza kuhusu Naba al-Adhim (Habari Kuu), na kwa hiyo jina la Sura. Suala kuu lililoangaziwa katika sura hii ya Qur'ani Tukufu ni ukweli kwamba Siku ya Kiyama ni hakika ambayo haiwezi kuepukika. Inatoa sababu za uhakika huo na inaeleza siku hiyo itakuwaje.

Awali sura inazungumza juu ya mfumo thabiti na imara unaotawala ulimwengu huu na inatoa mifano juu ya matukio ya asili kama mienendo ya ardhi, suala la viumbe kuumbwa kwa jozi, anga, usiku na mchana, mvua, ufufuo wa ardhi na anga. sheria zinazosimamia matukio haya. Kisha, inasisitiza kwamba Siku ya Kiyama itakuja na itakuwa miadi ya mwisho.

Surah An-Naba inazungumzia habari kubwa na tukio muhimu, yaani kuja kwa Siku ya Hukumu, na, ikitoa sababu za wazi na zisizoweza kupingwa, inasisitiza kwamba hakika itatokea.

Mwanzoni mwa Sura, watu wanaulizana kuhusu habari za Siku ya Kiyama. Kisha Mwenyezi Mungu anasema hivi karibuni watajifunza juu yake.

Surah An-Naba inazungumzia matukio ya Siku ya Kiyama na inaeleza hali za wafanyao wema na maovu siku hiyo. Inasema kwamba Siku ya Kiyama, watu wote wanaitwa kuhukumiwa mbele za Mwenyezi Mungu. Siku hiyo wale waliomuasi Mwenyezi Mungu katika dunia hii watachukuliwa kwenye adhabu iumizayo na wachamungu waliotenda mema katika dunia hii wataelekea kwenye baraka za milele.

captcha