IQNA

Mawaidha

Jinsi Nabii Ibrahim alivyowafunza watu kuhusu Mwenyezi Mungu

17:00 - May 09, 2023
Habari ID: 3476978
TEHRAN (IQNA) – Kwa kutumia aya za Qur’ani Tukufu, mwanachuoni wa Kiislamu anaeleza jinsi Nabii Ibrahim alivyomtambulisha Mwenyezi Mungu kwa watu wake.

Ayatullah Seyyed Mostafa Mohaghegh Damad, katika kikao cha tafsiri ya Qur'ani Tukufu, alibainisha baadhi nukta  kuhusu Surah Ash-Shu'ara. Zifuatazo ni nukuu za hotuba yake:

Mazungumzo kati ya Hadhrat Ibrahim na kabila lake ni ya kuvutia sana. Alichagua njia yenye kufundisha na yenye mambo fulani ambayo mtu anaweza kujifunza kwayo. Ibrahim anauliza baadhi ya maswali ili kuwafanya watu wafikiri. Kuuliza ni jambo muhimu katika kufikiri. Swali lake la kwanza lilikuwa wanaabudu nini? Ibrahim ni mhubiri wa imani ya Mungu mmoja lakini anaanzia hapa. Inaonekana kwamba swali hili liliwafanya wafikiri, na wakasema wanaabudu masanamu na daima wanayanyenyekea. Swali la pili ambalo Hadhrat Ibrahim aliuliza lilikuwa iwapo masanamu 'Yanakusikieni mnapo yaita? Hili ni swali gumu. Swali la tatu lilikuwa je, yanakufaeni, au yanakudhuruni? 

"Wakasema: Bali tumewakuta baba zetu wakifanya hivyo hivyo.” (Sura Ash-Shu'ara, aya ya 72)

Njia bora ya kumwabudu Mungu ni kuzungumza naye kupitia maombi au Dua. Kwa hakika dua inamaanisha kuita na kusikia jibu. Mtu anapaswa kuabudu Mungu ambaye anaweza kuzungumza naye. Qur’ani Tukufu inasisitiza kwamba watu wanapaswa kuzungumza na Mwenyezi Mungu, kwa hiyo inasema: “Wanapokuuliza waja wangu kuhusu Mimi, mimi niko karibu.  Na waja wangu watakapo kuuliza khabari zangu, waambie kuwa Mimi nipo karibu. Naitikia maombi ya mwombaji anapo niomba. Basi na waniitikie Mimi, na waniamini Mimi, ili wapate kuongoka.” (Surah Al-Baqarah, aya ya 186)

captcha