IQNA

Hujuma ya kigaidi

Raisi: Iran itatoa jibu kali na la kujutisha kwa wahusika wa hujuma ya kigaidi Shiraz

20:00 - October 27, 2022
Habari ID: 3475993
TEHRAN (IQNA)- Rais wa Iran amesema Jamhuri ya Kiislamu itatoa jibu kali na la kujutisha kwa wale waliohusika katika shambulio la kigaidi dhidi ya Haram Tukufu ya Shah Cheragh mjini Shiraz, kusini magharibi mwa nchi.

Rais Ebrahim Raisi alisema hayo Jumatano, muda mfupi baada ya kutokea shambulio hilo la kigaidi lililoua na kujeruhiwa makumi ya watu. Rais wa Iran amesisitiza kuwa: Shambulio hilo la kikatili halitapita hivi hivi bila ya kujibiwa. 

Sayyid Ebrahim Raisi ameeleza bayana kuwa, "Vikosi vya usalama na sheria vya nchi hii baada ya kutambua mzizi wa jinai hiyo ya kihaini, vitatoa jibu mwafaka kwa wapangaji na watekelezaji (wa jinai hiyo)."

Ameeleza kuwa, "uzoefu unaonesha kuwa, maadui wa Iran wanalipiza kisasi kwa kufeli njama zao za kuibua migawanyiko miongoni mwa jamii zilizoshikamana za Wairani."

Rais Raisi amesema maadui wa Jamhuri ya Kiislamu hivi sasa wamegeukia mbinu za ghasia na ugaidi kujaribu kukwamisha ustawi na maendeleo hapa nchini.

Watu wasiopungua 15 wameuawa huku 27 wakijeruhiwa katika shambulio hilo la kigaidi la jana Jumatano mwendo wa saa 12 kasorobo kwa saa za hapa nchini, katika Haram Tukufu ya Shah Cheragh mjini Shiraz, katika mkoa wa Fars kusini magharibi mwa nchi.

4094764

captcha