IQNA

Qur'ani Tukufu Inasemaje/25

Kinachogeuza Uadui kuwa Urafiki

15:56 - August 23, 2022
Habari ID: 3475670
TEHRAN (IQNA) - Hasira ni miongoni mwa hisia zinazosababisha uadui na kupelekea kuibuka matokeo mabaya ya kijamii. Uadui au uhasama unaweza kupunguzwa kwa njia fulani, lakini kuugeuzaa kuwa urafiki wa kindani ni jambo ambalo linaonekana kuwa lisilowezekana.

Hata hivyo hali hiyo, inaweza kupatikana kwa muujiza wa Neno la Mwenyezi Mungu.

Kuna aya katika Sura Fussilat ya Qur'ani Tukufu inayoonyesha jinsi ya kufanya hivyo: "Mema na maovu hayalingani. Pinga uovu kwa lilio jema zaidi. Hapo yule ambaye baina yako naye pana uadui atakuwa kama rafiki jamaa wa kukuonea uchungu." (Sura Fussilat, aya ya 34)

Kwanza, tunapaswa kuona nini aya hii inamaanisha nini inaposema 'maadui', kwani kuna uadui wa aina tofauti. Kuna uadui ambao umejikita katika ujinga, maadui wengine wamejikita katika husuda na wengine hutokana na shaka. Uadui wa aina hii unaweza kugeuzwa kuwa urafiki kwa mujibu wa aya hii, na sio wale ambao wamejikita katika ukafiri na nia ya kuharibu ukweli.

Aya inawausia watu kujibu maovu kwa vitendo vizuri na wakatae kulipiza kisasi. Katika Dua ya Makarim al-Akhlaq, Imam Sajjad (AS) anamuomba Mwenyezi Mungu amjaalie baraka za kuzungumzia kheri za watu na kuwasamehe wanapomsema vibaya. Kuna matukio mengi ya aina hiyo katika Sira ya Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) na watu wa nyumba yake yaani Ahl-ul-Bayt (AS) ambapo tabia na hulka yao njema  imewageuza maadui kuwa marafiki na wafuasi.

Kwa kuzingatia aya hii na nyinginezo za Surah Fussilat, hivi ndivyo tunavyopaswa kutenda ili kubadilisha maadui kuwa marafiki:

  1. Jibu tabia mbaya kwa wema: " Pinga uovu kwa lilio jema zaidi,..." ((Sura Fussilat sehemu ya aya ya 34).
  2. Watafutie wengine kheri na jueni kwamba Mwenyezi Mungu ametuumbia sisi sote pepo, kwa sharti tukichagua kuingia humo: “Sisi ni vipenzi vyenu katika maisha ya dunia na katika Akhera, na humo mtapata kinacho tamaniwa na nafsi zenu, na humo mtapata mtakavyo vitaka. ” (Sura Fussilat aya ya 31)
  3. Daima tukumbuke kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe na Mwenye kurehemu: "Ni takrima itokayo kwa Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu." (Sura Fussilat aya ya 32)
  4. Kulingania kwetu kwa Mwenyezi Mungu kunafuata lengo lililo bora zaidi Mema na maovu hayalingani. "Na ni nani mbora wa kusema kuliko aitaye kwa Mwenyezi Mungu na akatenda mema, na akasema: Hakika mimi ni katika Waislamu? Mema na maovu hayalingani. Pinga uovu kwa lilio jema zaidi. Hapo yule ambaye baina yako naye pana uadui atakuwa kama rafiki jamaa wa kukuonea uchungu." (Sura Fussilat aya  ya 33-34)
  5. 5. Muujiza huo wa kubadilisha uadui kuwa urafiki hupatikana kwa maneno mazuri na matendo mema na unahitaji subira na ustahmilivu. “Lakini hawapewi wema huu ila wanao subiri, wala hawapewi ila wenye bahati kubwa.” (Sura Fussilat aya ya 35)
Habari zinazohusiana
captcha