IQNA

Qur’ani inasemaje/ 8

Qur’ani Tukufu inasisitiza kuwaheshimu, kuwaenzi wazazi

20:29 - June 17, 2022
Habari ID: 3475389
TEHRAN (IQNA) - Kuheshimu wazazi ni mojawapo ya mafundisho makuu ya maadili ya Uislamu na Qur’ani inalipa suala hili umuhimu mkubwa sana.

Wazazi ndio wanaomwezesha mtu kuingia na kuishi katika dunia hii na baada ya kuzaliwa kumlea mtoto kwa uangalifu mkubwa na wema, wakimpatia mtoto chochote wanachoweza.

Mtu yeyote akitufanyia jambo jema, tunaona kuwa ni jambo la lazima kumthamini na kumshukuru. Kwa hiyo, wazazi, ambao hujitolea muhanga vingi maishani ili kuwalea watoto wao ndio wanaostahili zaidi kuthaminiwa na kushukuriwa.

Qur’ani Tukufu katika aya kadhaa inataja haja ya kuwathamini wazazi sambamba na kumshukuru Mwenyezi Mungu na inawaamrisha watu kuwaheshimu na kuwafanyia wema wazazi baada ya kuamrisha Tauhidi ambayo ndio msingi wa dini. Hii inaonyesha umuhimu mkubwa ambao Qur’anI inalipa suala hili:

Katika sehemu ya aya ya 38 ya Sura al Baqarah katika Qur’ani Tukufu tunasoma hivi:

“…Hamtamuabudu yeyote ila Mwenyezi Mungu; na muwafanyie wema wazazi…” 

 

Aidha katika ya sehemu ya aya ya 14 ya Sura Luqman  tunasoma hivi:

“… Nishukuru Mimi na wazazi wako. Ni kwangu Mimi ndiyo marudio.”

Tunapokua wakubwa wakati inaonekana  hatuhitaji tena msaada na msaada wa wazazi wetu, bado ni muhimu kuwashukuru? Je, bado wanastahili kuheshimiwa wanapozeeka na hawawezi tena kutusaidia?

Qur’an inaashiria hili katika aya ya 23 ya Sura Al-Isra: Na Mola wako Mlezi ameamrisha kuwa msimuabudu yeyote ila Yeye tu, na wazazi wawili muwatendee wema. Mmoja wao akifikia uzee, naye yuko kwako, au wote wawili, basi usimwambie hata: Ah! Wala usiwakemee. Na sema nao kwa msemo wa hishima.”

Kuwatendea mema wazazi kunaweza kuwa kupitia msaada wa kifedha, kisaikolojia au kiroho. Mtukufu Mtume Muhammad SAW aliulizwa kama mtu anaweza kuwafanyia wema wazazi baada ya kifo chao. Mtume SAW alijibu hivi: “Ndio, kwa kuwaombea dua na kuwaombea msamaha kwa Mwenyezi Mungu, kuwalipia deni zao na kuwaheshimu marafiki zao”.

Katika Tafsiri yake ya Nur ya Qur’ani Tukufu, Sheikh Muhsin Qara'ati anataja nukta kadhaa kuhusu aya hii:

1- Tauhidi  ni inaongoza katikaamri zote za Mwenyezi Mungu: “Mola wenu amekuamrisheni msimuabudu yeyote isipokuwa Yeye tu.”

2- Kuwatumikia wazazi wa wazazi na kuwafanyia wema ni tabia ya wenye itikadi ya kweli ya Tauhidi  “… na (amekuamrisha) kuwafanyia wema wazazi wako.”

3- Wazazi hawahitaji kuwa Waislamu ili kuhudumiwa na kuheshimiwa. Unapaswa kuwatii isipokuwa tu pale wanaopkuamuru umuasi Mwenyezi Mungu.

4- Qur’an inawaamrisha watoto kuwaheshimu na kuwatumikia wazazi wao lakini haiwaamrishi wazazi kuwafanyia wema watoto wao kwa sababu wao wanafanya hivyo kutokana na dhati yao kama wazizi.

5- Kadiri wazazi wanavyodhoofika kimwili na kisaikolojia, ndivyo itakavyokuwa muhimu zaidi kuwasaidia na kuwafanyia wema: “Ikiwa mmoja wao au wote wawili watafikia uzee…”

6- Hatupaswi kuwaacha wazazi wetu wa zamani kwenye nyumba za wazee bali tunapaswa kuwa pamoja nao.

7- Sio tu kuwafanyia wema bali pia kuzungumza nao vizuri ni muhimu: “… semeni nao kwa maneno ya hishima.”

8- Iwapo hawakukuheshimu na hawakusema nawe vizuri, bado unahitaji kuwaheshimu: “Sema nao kwa maneno ya hishima.”

captcha