Kwa mujibu taarifa, maonyesho hayo yanaonyesha shughuli za Kituo cha Uchapishaji Qur’ani cha Mfalme Fahd.
Wanaotembelea maonyesho hayo wanashuhudia mchakato mzima wa uchapishaji na usambazwaji Qur’ani Tukufu pamoja na teknolojia inayotumika katika uchapishaji.
Maonesho hayo ambayo yamezinduliwa Alhamisi na Idara ya Masuala ya Kidini ya Asir yanatazamiwa kuendelea kwa muda wa siku 10.
Kituo cha Uchapishaji Qur’ani cha Mfalme Fahd kiko katika mji wa Madina na mbali na Misahafu ya Kiarabu pia huchapisha tarjuma za Qur’ani kwa lugha 40. Kituo hicho huchapisha Misahafu karibu milioni 10 kwa mwaka.
3480058