IQNA

Kadhia ya Palestina

Qari wa Algeria asoma aya za Qur'ani kwa heshima kwa watu wa Gaza (+Video)

16:26 - April 21, 2024
Habari ID: 3478712
IQNA - Picha za qari wa Algeria akisoma Qur'ani kwa ajili ya kuwaenzi watu wa Gaza zimesambaa katika mitandao ya kijamii.

Qari wa Algeria asema aya za Qur'ani kwa heshima kwa watu wa Gaza (+Video)Katika video hii, Ali Dqaa anasoma aya kutoka katika Kitabu Kitakatifu na kisha anawaombea ushindi watu wa Ukanda wa Gaza.

Anasoma Aya ya 5 ya Sura ya Israa:

 Basi itapo fika ahadi ya kwanza yake tutakupelekeeni waja wetu wa kali kwa vita. Watakuingilieni ndani ya majumba. Na hii ilikuwa ahadi iliyo timizwa."

Utawala wa Israel ulianzisha mashambulizi ya mauaji ya kimbari dhidi ya Ukanda wa Gaza mnamo Oktoba 7, 2023.

Zaidi ya Wapalestina 34,000, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, wameuawa huko Gaza, na wengine zaidi ya 76,800 wamejeruhiwa katika kampeni hiyo ya ukatili wa utawala dhalimu wa Israel.

4211402

 

Kishikizo: gaza algeria
captcha