IQNA

Watu 4,000 kushiriki Itikafu katika Masjid an-Nabawi, mjini Madina

22:08 - April 22, 2022
Habari ID: 3475156
TEHRAN (IQNA)- Msikiti Mtakatifu wa Mtume SAW, Masjid an-Nabawi, mjini Madina umesajili watu 4,000 watakaoshiriki katika Itikafu wakati wa siku 10 za mwisho za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Katika siku hizo ambazo ni katika siku za usiku wa cheo au Laylatul Qadr waumini hutumia wakati wao wote wakiwa katika Sala, dua na usomaji Qur’ani Tukufu.

Kwa mujibu wa taarifa, watakaoshiriki katika Itikaf watapata  futari na daku pamoja na huduma zinginezo katika kipindi chote cha Itikafu katika Masjid an-Nabawi, mjini Madina.

Mwezi uliopita Wakuu wa Saudi Arabia walitangaza kuwa wanaruhusu tena ibada ya Itikafu katika Misikiti Miwili Mitakatifu ambayo ni Msikiti Mtakatifu wa Makka, Al Masjid Al Haram, na halikadhalika katika Msikiti Mtakatifu wa Mtume SAW, Masjid an-Nabawi, mjini Madina.

Kabla ya kuzuiwa kwa muda kutokana na janga la corona, karibu waumini laki moja walikuwa wakishriki katika Itikafu katika misikiti hiyo miwili wakati wa siku 10 za mwisho za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

mijumuiko mkiubwa ya futari itaruhusiwa tena katika Misikiti Miwili Mitakatifu katika mwezi mtukufu wa Ramadhani baada ya kuzuiwa kwa muda wa miaka miwili kutokana na janga la corona.

3478589

Kishikizo: madina itikafu ramadhani
captcha