Sayyid Abdul Malik Badruddin Al-Houthi alisema hayo katika hotuba yake kupitia televisheni usiku wa kuamkia leo na kueleza kuwa: Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu ndizo zinazotekeleza uvamizi huo wa Marekani, Israel na Uingereza.
Amesema misingi ya vita dhidi ya Yemen ni hulka na mienendo ya jinai, na uvamizi huo umelenga sekta zote za taifa hilo maskini la Kiarabu, mbali na kumwaga damu za Wayemen.
Sayyid Abdul Malik Badruddin Al-Houthi ameongeza kuwa, Yemen inakabiliwa na vita shadidi vya kiuchumi vinavyolenga kuharibu na kusambaratisha rasilimali zote za nchi hiyo, na kuitaabisha kila familia ya Yemen.
Moto wa vita uliowashwa na Saudi Arabia na washirika wake dhidi ya Yemen kuanzia mwezi Machi 2015 na kuendelea hadi sasa umeshapelekea mamia ya maelfu ya watu wasio na hatia kupoteza maisha, mbali na kuwaacha wengine zaidi milioni nne wakiwa hawana pa kuishi.
Uchokozi na uvamzi wa kijeshi wa Saudia dhidi ya Yemen umebomoa na kuharibu zaidi ya asilimia 85 ya miundombinu ya nchi hiyo masikini zaidi katika Bara Arabu na kuisababishia pia uhaba mkubwa wa chakula na dawa nchi hiyo ya Waislamu.
3478271