IQNA

Baada ya Israel kumwaga damu ya Wapalestina Ghaza, yaidhinishwa kufungua ubalozi Abu Dhabi

18:50 - June 30, 2021
Habari ID: 3474058
TEHRAN (IQNA)- Wiki kadhaa baada ya utawala wa Kizayuni wa Israel kuua idadi kubwa ya wanawake, watoto na raia wa Palestina katika Ukanda wa Ghaza, utawala huo haramu umekaribishwa katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na kufungua ofisi za kibalozi mjini Abu Dhabi.

Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) umeendeleza usaliti wake kwa kadhia ya Palestina kupitia kufungua rasmi ubalozi wa utawala wa Kizayuni mjini Abu Dhabi.

Siku ya Jumanne,  Yair Lapid, Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel akiitembelea UAE, ambapo amefungua rasmi ubalozi wa utawala huo wa Kizayuni katika mji mkuu Abu Dhabi, na pia ubalozi mdogo wa utawala huo pandikizi mjini Dubai, licha ya kuanza kufanya kazi miezi mitano iliyopita.

Mapema mwezi huu, UAE ilifungua rasmi ubalozi wake mjini Tel Aviv, siku chache tu baada ya dunia kushuhudia jinai na mauaji ya kutisha ya zaidi ya Wapalestina 250 wa Ukanda wa Gaza, yaliyofanywa na jeshi katili la Israel. 

Umoja wa Falme za Kiarabu Septemba mwaka jana ilianzisha uhusiano rasmi na utawala wa Kizayuni wa Israel, ikiwa ni nchi ya kwanza ya Kiarabu jkufanya hivyo baada ya kipindi cha miaka 26. Baadhi ya tawala za Kiarabu kama Sudan, Bahrain na Morocco zimefuata mkumbo huo kibubusa.

Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina amejibu kitendo cha Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) cha kufungua rasmi ubalozi wa utawala wa Kizayuni mjini Abu Dhabi na kusema kuwa, makubaliano ya uhusiano wa kawaida kati ya nchi za Kiarabu na Israel kamwe hayawezi kuleta utulivu na amani.

Rais huyo wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina ameongeza kuwa, dunia hivi sasa inashuhudia uhakika wa dola la Israel na inaona jinsi utawala huo ulivyo vamizi na mbaguzi za kizazi.

/3475104

captcha