IQNA

Watetezi wa Palestina

Kikao cha ICJ kuhusu jinai za Israel huko Gaza, Wapalestina wapongeza Afrika Kusini

22:14 - January 11, 2024
Habari ID: 3478184
IQNA-Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) imeanza kusikiliza shauri la kesi iliyofunguliwa na Afrika Kusini dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel, ambayo inaishutumu kwa kufanya mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina wa Gaza.

Kufuatia kuendelea jinai za utawala wa kibaguzi wa Israel dhidi ya Wapalestina wasio na hatia, wiki iliyopita Afrika Kusini iliushtaki rasmi utawala huo katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki huko The Hague.

Mashtaka muhimu ya Afrika Kusini ni jinai za kivita, mauaji ya kizazi na kikabila huko Gaza na katika maeneo mengine ya ardhi zinazokaliwa kwa mabavu ya Palestina.

Katika shauri lake hilo la mashtaka, Afrika Kusini inataka ICJ kuilazimisha Israel kusitisha operesheni zake za kijeshi huko Gaza, ambapo inasema Israel inafanya mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina, na ICJ iyazingatie matendo ya Israel kwenye ardhi hiyo ya Wapalestina chini ya Mkataba wa Kimataifa wa kuzuia mauaji ya kimbari uliopitishwa mwaka 1948.

Afrika Kusini ni miongoni mwa nchi za Kiafrika ambazo tokea yalipoanza mashambulizi ya kigaidi ya Israel dhidi ya Wapalestina zimetoa radiamali na kulaani hatua hizo za kinyama za Wazayuni dhidi ya wananchi wasiokuwa na ulinzi wa Gaza. Aghalabu ya nchi hizo ambazo zilitawaliwa kwa miaka mingi na nchi za Magharibi na kukumbana na ukoloni, unyonyaji na ubaguzi wa rangi sambamba na kulaani jinai za Israel, zimetaka kukomeshwa ukatili unaofanyiwa wananchi wanaozingirwa wa Gaza

Wapalestina wapongeza Afrika Kusini

Wapalestina jana Jumatano walikusanyika katika uwanja wa mwendazake mzee Nelson Mandela huko Ramallah lengo likiwa ni kuishukuru Afrika Kusini kwa hatua yake ya kuwasilisha kesi katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) dhidi ya utawala haramu wa Israel.

Wapalestina wakusanyika katika uwanja wa Mandela Ramallah kuishukuru Afrika Kusini kuhusu kesi ya ICJ

Washiriki katika mkusanyiko huo walikuwa wamebeba mabango yenye maandishi yanayotaka kusitishwa vita haraka iwezekanavyo huko Ukanda wa Gaza. Mandela alilinganisha hali mbaya na masaibu waliyonayo Wapalestina wa Ukanda wa Gaza na wa Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan kuwa sawa na waliyopitia  raia weusi wa Afrika Kusini wakati wa utawala wa ubaguzi wa rangi nchini humo wa Apartheid. 

Issa Kassis Meya wa mji wa Ramallah katika Ukingo wa Magharibi alitoa shukrani katika mkusnayiko huo akisema:" Leo tunamshukuru Nelson Mandela, tunaishukuru Afrika Kusini." Amesema, tunaishukuru Afrika Kusini kwa kuwasilisha kesi katika mahakama ya ICJ kuhusu jinai za kivita za Israel huko Ukanda wa Gaza, na tunaamini kuwa nchi nyingi zimehisi machungu na maumivu yetu lakini Afrika Kusini iliamua kuchukua hatua na kuwasilisha kesi dhidi ya utawala wa Kizayuni katika mahakama ya ICJ. 

4193378

Habari zinazohusiana
captcha