IQNA

Wamisri wakaribisha mpango wa Qur'ani wa Wizara ya Wakfu

Wamisri wakaribisha mpango wa Qur'ani wa Wizara ya Wakfu

16:18 - December 06, 2023
Habari ID: 3477994
TEHRAN (IQNA) - Mpango uliozinduliwa katika misikiti ya Misri kwa ajili ya kurekebisha makosa yanayofanywa na watu wakati wa kusoma Qur'ani Tukufu umepokelewa vyema, maafisa wanasema.

Mpango huo unaojulikana kama  "Sahihisha Kisomo Chako", unafanyika katika misikiti kadhaa mikubwa katika miji tofauti.

Misikiti kumi ni mwenyeji wa utekelezaji wa mpango huo.

Wa kwanza alikuwa Msikiti wa Sayyidah Zaynab mjini Cairo Alhamisi iliyopita.

Siku ya Jumatatu jioni, Msikiti wa Al-Nasr huko Arish, Mkoa wa Sinai Kaskazini, uliandaa hafla hiyo. Ilihudhuriwa na idadi kubwa ya watu.

Sheikh Mahmoud Marzouq, mkurugenzi wa Idara ya Wakfu ya gavana, alipongeza mapokezi mazuri ya mpango huo, ambapo, alisema, watu husoma robo ya Hizb ya Qur'ani kila siku.

Kila siku baada ya sala ya Maghrib na Isha, Imamu wa Sala katikamsikiti au mtaalamu wa kusoma Qur'ani husoma aya za Qur'ani, kuanzia Surah Al-Fatiha, Sura ya kwanza ya Kitabu Kitukufu, na watu wanarudia aya moja baada ya nyingine, Marzouq alibainisha.

Mpango huo unalenga kutumikia Qur'ani Tukufu, kuwahimiza watu kurekebisha usomaji wao , na kuhimiza watu zaidi kwenda misikitini, Wizara ya Waku imesema.

4186006

Habari zinazohusiana
captcha