IQNA

Mbinu ya Elimu ya Manabii; Ibrahim / 6

Nabii Ibrahimu ( AS) anatumia Tawbah kama Njia Kuu ya Kuelimisha

17:47 - June 19, 2023
Habari ID: 3477162
Kila mtu anaweza kufanya makosa au kutenda dhambi, Mwenyezi Mungu kupitia dini, ametoa wito kwa wanadamu kutubu na kutafuta msamaha ili kufidia dhambi na makosa yao.

Tawbah (toba) ni njia ya kielimu na kuzingatia vipengele vyake tofauti itakuwa ya kuvutia.

Kujua kwamba kwa kutubu, mtu anaweza kufidia dhambi yake kutafanya iwe rahisi kwake kukana dhambi. Lakini toba si tu kwa mtu amefanya dhambi, Inafaa kwa mtu kutubu hata kama hakuna dhambi iliyotendwa. Imamu Sadiq (AS) alisema sala bora zaidi ni Istiqfar kuomba msamaha kwa  Mwenyezi Mungu. Jambo moja kuhusu Tawbah ni kwamba mwalimu hatakiwi kumuacha mwanafunzi wake pale mwanafunzi anapokosea. Jambo la kwanza ambalo mwalimu anapaswa kufanya ni kujaribu kumfanya mwanafunzi atambue kosa lake kisha kukubali msamaha wake, Bila haya, haingekuwa na athari ya kielimu.Nabii  Ibrahimu (AS), kama nabii  wa  Mwenyezi Mungu, alitumia njia hii ya elimu.

Ibrahim (AS) alimuomba Mwenyezi Mungu kuhusu yeye na mwanawe Ismail (AS); Mola wetu, Tuonyeshe ibada zetu na tukubalie Tawbah zetu Wewe ni Mwingi wa kupokea toba, Mwenye kurehemu,Tafsiri ya  Aya ya 128 ya Surati  Al-Baqarah.

Kwa mujibu wa Allamah Tabatabaei katika Ufafanuzi wa Al-Mizan wa Quran Tukufu  kwa toba,Nabii  Ibrahim na Ismail (AS)  walitaka kumkaribia Mwenyezi  Mungu, Anaamini kwamba neno Tawbah katika Tafsiri ya Aya hii maana yake ni kurudi.

Mwenyezi Mungu anasema katika Tafsiri ya  Aya ya 4 ya Surati Al-Mumtahanah; Nyinyi mna mfano mzuri kwa Nabii  Ibrahim (AS) na walio pamoja naye. Wakawaambia kaumu yao; Sisi tumejitenga nanyi na hayo mnayo yaabudu badala ya Mwenyezi Mungu, Sisi tunakukadhibisha, uadui na chuki zimedhihiri baina yetu milele mpaka muamini Mwenyezi Mungu peke yake,  Isipokuwa  Nabii Ibrahim (AS) alimwambia baba yake; Hakika mimi nitakuombea msamaha ingawa sina uwezo wa kufanya chochote kwako na kwa  Mwenyezi Mungu  Mola wetu sisi tumekutegemea Wewe; Kwako tunaelekea, na Kwako ndio Tunarejea.

 

3483989

captcha