IQNA

Mwezi wa Ramadhani

Maeneo matakatifu huko Makka, Madina kukaribisha waabudu Milioni 3 Mwezi wa Ramadhani

17:14 - March 04, 2023
Habari ID: 3476656
TEHRAN (IQNA)-Mpango mkubwa wa kuwahudumia waumini wapatao milioni 3 katika maeneo matakatifu zaidi ya Kiislamu katika mwezi mtukufu wa Ramadhani unaokuja ulizinduliwa nchini Saudi Arabia.

Mpango huo ulitangazwa na Abdul Rrahman Al Sudais, mkuu wa Urais Mkuu wa Masuala ya Misikiti Miwili Mitakatifu huko Makka na Madina.

Mpango huo wa operesheni unasimamiwa na wafanyikazi 12,000 watakahudumu masaa 24 kuhudumia waumini milioni 3 katika misikiti yote miwili, afisa huyo alisema.

Mpango huo unaoitwa "kutoka kuwasili hadi kufikia", unazingatia safari waumini punde wanapowasili maeneo mawili matakatifu. Waumini watasaidiwa kuzunguka au kutufu Kaaba Tukufu katika Msikiti Mkuu wa Makka na kutembea kati ya vilima viwili vya Safa na Marwah ambazo ni ibada muhimu za Umra au Hija ndogo, pamoja na kuswali sala za kila siku na itikafu.

Kulingana na afisa hiyo, mpango huo umeundwa ili kuwezesha ibada ya kuzunguka Kaaba Tukufu kwa karibu Mahujaji 107,000 wa Umrah kwa saa.

Ramadhani, inayotarajiwa kuanza mwaka huu tarehe 23 au 24 Machi, huwa ndiyo msimu wa kilele wa Umrah na huadhimishwa kwa kukithirishwa ibada.

3482690

Kishikizo: umrah ramadhani saudais
captcha