IQNA

Sura za Qur'ani Tukufu/29

Qur'ani inafananisha kuabudu miungu ya uongo na Mtandao wa Buibui

11:11 - September 06, 2022
Habari ID: 3475740
TEHRAN (IQNA) – Mitume wa Mwenyezi Mungu walijaribu kuonyesha jinsi miungu ya uongo isiyo na thamani lakini walikabili ukaidi wa wafuasi wao wengi. Surah Al-Ankabut katika Qur'ani Tukufu inalinganisha imani za watu hao waliopotoka na utando wa buibui.

Jina la Sura ya 29 ya Quran ni Al-Ankabut (buibui) kutokana na mdudu huyo ambaye ametajwa katika aya ya 41 ya sura hiyo.

Katika aya hii, kitendo cha makafiri cha kuabudu miungu au masanamu kinafananishwa na kutegemea utando wa buibui: “Mfano wa walio wafanya walinzi badala ya Mwenyezi Mungu, ni mfano wa buibui alivyo jitandia nyumba. Na hakika nyumba dhaifu mno kuliko zote ni jumba la buibui, laiti kuwa wanajua."

Inasemekana katika tafsiri ya Aya hii kwamba ulinganisho huo unalenga kuonyesha kuwa kuabudu masanamu hakuna faida kwa makafiri na hakuwezi kuwaepusha na madhara na matatizo.

Sehemu ya kwanza ya Sura inahusu suala la mtihani wa Mwenyezi Mungu na hadhi ya Munafiqeen (wanafiki). Masuala haya mawili yanahusiana kwa sababu kumjua mnafiki haiwezekani bila ya kumjaribu.

Sehemu nyingine ya sura inazungumzia Tauhidi na dalili za Mwenyezi Mungu duniani pamoja na kupigana na Shirki (ushirikina).

Sehemu ya mwisho ya Sura Al-Ankabut inaeleza kwa kina juu ya udhaifu na kutokuwa na uwezo wa miungu na masanamu, ikisema huonekana madhubuti na wagumu lakini hawawezi kutatua matatizo. Pia inazungumzia utukufu wa Quran na ukweli wa Mtukufu Mtume (SAW).

 

Habari zinazohusiana
captcha