Aplikesheni hiyo imezinduliwa na Sheikh Ali Hassan Ghaloum na inajumuisha maamurisho ya kidini na masuala ya kifiqhi ambayo yametajwa katika Qurani Tukufu.
Aidha aplikesheni hiyo ina taarifa mbali mbali za Qurani kama vile ibara za Qur'ani na maneneo yanayoshabihiana na halikadhalika maelezo kuhusu aya. Aidha aplikesheni hiyo inabaini sura zilizoteremshwa Makka na Madina.
Applikesheni hiyo inaweza kupakuliwa katika aahkam.com au play store kwa simu za mfumo wa Android.
Kwa maelezo zaidi kuhusu utumizi wa aplikesheni hiyo unaweza kutembelea https://youtu.be/XEJtf4o0wtQ