IQNA

Amali za usiku wa Lailatul Raghaib

15:45 - February 18, 2021
Habari ID: 3473660
TEHRAN (IQNA) – Leo ni Lailatul Raghaib ambao ni usiku wa kuamkia Ijumaa ya kwanza ya Mwezi wa Rajab.

Usiku wa Lailatul Raghaib umetajwa kuwa miongoni mwa nyakati bora zaidi ambazo Mwenyezi Mungu SWT hujibu Dua za waja Wake.

Inadokezwa kuwa katika usiku huu Malaika wanashuka ardhini kwa lengo la kuchukua ujumbe wa waja wema wenye Ikhlasi na kuufikisha kwa Mwenyezi Mungu SWT.

Kwa hivyo usiku huu ni kati ya nyusiku bora ambazo Mja anaweza kumuomba Mwenyezi Mungu amneemeshe kwa neemba mbali mbali na moja ya neema hizo wakati huu ni afya na salama.

Katika usiku huu inapendekezwa kuswali sala ya Salatul Laylatul Raghaib. Sala hii ina rakaa 12, katika kila rakka unasoma Al Fatiha na Suratul Qadir mara 3 na Suratul Ikhlas mara 12, inaswaliwa kama swalatu Fajir. Halikadhalika inaswaliwa Mufrad na sio jamaa.

Kisha baada ya kukamilisha Sala kuna dhikri ifuatayo ambayo husomwa mara sabini

اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَی مُحَمَّدٍ النَّبِیِّ الْأُمِّیِّ وَ عَلَی آلِهِ

Kisha baada ya hapo muumini akiwa katika hali ya kusujudu husoma dhikri ifuatayo

سُبُّوحٌ قُدُّوسٌ رَبُّ الْمَلائِکةِ وَ الرُّوحِ

Baada ya kuinuka kutoka sijda muumini anatakiwa kusoma mara sabini dhikri ifuatayo

رَبِّ اغْفِرْ وَ ارْحَمْ وَ تَجَاوَزْ عَمَّا تَعْلَمُ إِنَّک أَنْتَ الْعَلِی الْأَعْظَم

Mwenye kuswali Salatul Lailatul Raghaib  husamehewa madhambi mengi hata yale mazito. Kwa msingi huo ni usiku uliojaa fursa kwa kila mja kujikurubisha kwa Mola Mlezi.

/3954771

Kishikizo: rajab Lailatul Raghaib
captcha