IQNA

Mafundisho ya Qur’ani kwa njia ya intaneti nchini Lebanon

22:09 - September 14, 2020
Habari ID: 3473169
TEHRAN (IQNA) – Mafundisho ya Qur’ani kwa njia ya intaneti yameandaliwa na Kituo cha Darul Qur’an nchini Lebanon. Kituo hicho kinafungamana na Mfawidhi wa Haram Takatifu ya Imam Hussein AS.

Kwa mujibu wa taarifa, Sayyed Ali Abul-Hassan, Mkuu wa Darul Qur’an tawi la Lebanon amesema mafunzo hayo ya Qur’ani Tukufu yaliwalenga mamia ya wavulana na washichana katika msimu wa joto mwaka huu.

Ameongeza kuwa washiriki kutoka makundi mbali mbali ya umri walishiriki kutoka miji mikubwa na midogo zaidi ya 15.

Kozi hiyo ilijumuisha kusoma na kuhifadhi Qur’ani Tukufu  na pia mashindano ya Qur’ani yaliyopewa jina la Al Ghadira. Washiriki bora walipata zawadi za fedha taslimu katika sherehe ya kuhitimisha kozi hiyo.

3922701

 

captcha