Sheikh Azzam Khatib, Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Wakfu ya Jordan mjini Quds amesema sheria kali za kiafya zimewekwa kutokana na ongezeko la idadi ya walioambukziwa COVID-19 mjini Quds na miji mingine ya Wapalestina.
Amesema wamechukua hatua hiyo ili wasilaumiwa kuhusika katika kueneza COVID-19 katika mji wa Quds ambao unakaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni wa Israel. Msikiti wa Al Aqsa ulikuwa umefungwa kwa muda wa miezi miwili hadi Mei 25 ikiwa ni katika hatua za kuzuia kuenea ugonjwa wa COVID-19.