IQNA

China ihimizwe isitishe sera za chuki dhidi ya Uislamu +Video

15:20 - June 02, 2020
Habari ID: 3472825
TEHRAN (IQNA) – China inapaswa kuhimizwa isitishe sera zake cha chuki dhidi ya Waislamu hasa zile zinazowashusu Waislamu wa jamii wa Uighur.

Akitoa wito huo kwa njia ya video, Dr. Massoud Shajareh, Mkuu wa Tume ya Kiislamu ya Haki za Binadamu (IHRC) yenye makao yake London amesema China inapaswa kuheshimu haki za kimsingi za Waislamu waliowachache nchini humo.

Uislamu ni kati ya dini tano ambazo zinatambuliwa rasmi na Chama cha Kikomunisti China ambapo kuna takribani Waislamu milioni 23 nchini humo.

Katika miaka ya hivi karibuni kumeongezeka sera za kuwakandamiza Waislamu katika nchi hiyo hasa katika jimbo la Xinjiang wenye Waislamu Zaidi ya milioni 10 kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi na misimamo mikali.

Kwa mujibu wa wataalamu wa haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa, Waislamu takribani milioni moja wa jamii ya Uighur wanashikiliwa katika kambi za kuwafunza Usosholisti wa Kichina na wanalazimishwa kwa kisingizio cha kukabiliana na ugaidi.

Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Kuangamiza Ubaguzi wa Rangi imesema imeandika ripoti kuhusu masaibu ambayo Waislamu wanakumbana nayo katika kambi hizo.

3471581

captcha