IQNA

Balozi wa Syria katika Umoja wa Mataifa

Vikwazo vya Marekani na maradhi ya COVID-19 ni tishio kwa dunia

11:43 - May 11, 2020
Habari ID: 3472755
TEHRAN (IQNA)- Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Syria katika Umoja wa Mataifa amesema, ugaidi unaolenga siha za watu ni hatua mpya ya upande mmoja ya Marekani ambayo imeyaweka hatarini maisha ya watu bilioni mbili duniani.

Bashar al-Jaafari ameyasema hayo katika kikao kilichofanyika kwa njia ya mawasiliano ya inatenti kwa anuani ya "Vikwazo vya Marekani na maradhi ya Covid-19 - tishio kwa dunia" na akabainisha kwamba: Janga la mripuko wa corona limeizushia tatizo jipya serikali ya Syria.

Mwakilishi wa kudumu wa Syria katika Umoja wa Mataifa amesema: Kulingana na Hati ya Umoja wa Mataifa, kitu kinachotajwa kama vikwazo kiko kinyume cha sheria na si halali. Umoja wa Mataifa hauutambui mfumo wowote wa vikwazo unaowekwa na nchi.

Al-Jaafari ameongeza kuwa: Viongozi wa Marekani wamejuzisha silaha na fedha zinazotolewa na nchi za eneo la Ghuba ya Uajemi kwa makundi ya kigaidi kaskazini mashariki na kaskazini magharibi mwa Syria na wanalitambua hilo kama misaada ya kibinadamu.

Balozi wa Syria katika Umoja wa Mataifa amesisitiza kuwa: " Sisi tunavitambua vikwazo vinavyotekelezwa dhidi ya nchi 39 kuwa ni 'ugaidi dhidi ya siha'. Hapo kabla nchi za Magharibi zilitekeleza ugaidi wa kisiasa, fedha, elimu, vyombo vya habari na uchumi; na hivi sasa vimegeukia 'ugaidi wa dhidi ya siha'.

3471405

captcha