IQNA

Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani ya Kuwait Kuanza Aprili 10

20:16 - March 28, 2018
Habari ID: 3471446
TEHRAN (IQNA)-Mashindano ya 9 ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Kuwait yanatazamiwa kuanza katika nchi hiyo ya Ghuba ya Uajemi mnamo Aprili 10.

TEHRAN (IQNA)-Mashindano ya 9 ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Kuwait yanatazamiwa kuanza katika nchi hiyo ya Ghuba ya Uajemi mnamo Aprili 10.

Kwa mujibu wa Waziri wa Wakfu na Masuala ya Kiislamu nchini Kuwait Sheikh Fahd al Afasi, idadi ya washiriki mwaka huu inatazamiwa kuwa zaidi ya miaka iliyopita.

Amesema moja ya malengo muhimu ya mashindano hayo ni kuwahimiza vijana kusoma Qur’ani Tukufu na kutafakari kuhusu mafundisho yake.

Affasi amesema mashindnao hayo halikadhalika yanalenga kustawisha tahami za Kiislamu huku kukiwa na sisitizo la kustawisha thamani za Kiislamu. Aidha amesisitiza umuhimu wa Qur’ani Tukufu na kuwaenzi watu wanaoihudumua Qur’ani Tukufu.

Mashindano  hayo yatafanyika katika kategoria za kuhifadhi na kusoma Qur’ani Tukufu.

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran tayari imetangaza itamtuma Qari Medhi Ghulamjeda na Hafidh Jawad Delfani katika mashindano hayo ya kimataifa ya Qur’ani ya Kuwait ambayo ni maarufu kama Zawadi ya Kuwait ya Qur’ani.

3702162

captcha