IQNA

UNESCO yakanusha taarifa bandia

15:07 - July 13, 2016
Habari ID: 3470453
Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) limeitaja kuwa bandia habari iliyoenezwa kuwa limeitaja dini tukufu ya Kiislamu kuwa ndiyo dini ya amani zaidi duniani.

Katika taarifa, UNESCO imeashiria madai ya hivi karibuni yaliyochapishwa na tovuti ijulikanayo kama juntakreporter iliyodai kuwa UNESCO imetoa cheti ikisema, "Uislamu ni dini ya Amani duniani."

UNESCO imesema haijawahi kutoa taarifa kama hiyo na kwamba cheti kilichochapishwa katika tovuti hiyo ni bandia. UNESCO imesema tovuti hiyo kwa kawaida huchapisha habari za vichekesho.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, "UNESCO haijawahi kuwa na uhusiano wowote na 'Taasisi ya Kimataifa kwa Ajili ya Amani', wala haijawahi kuunga mkono taarifa kama hiyo au kutoa cheti kama hicho."

UNESCO imesema jukumu lake ni kustawisha mazungumzo baina ya dini na baina ya tamaduni kote duniani kwa uungaji mkono wa nchi wanachama, washirika na mitandao.

Taarifa hiyo imesema UNESCO inaeneza heshima kwa usawa kwa dini na itikadi zote na daima inajitahidi kuimarisha na kukurubisha watu wote duniani kadiri inavyowezekana.

3514582

Kishikizo: unesco iqna uislamu
captcha