IQNA

Rouhani: Matakfiri wanalenga kuvurga umoja wa Waislamu

19:12 - June 28, 2015
Habari ID: 3320677
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelaani hujuma ya hivi karibuni ya kigaidi dhidi ya msikiti nchini Kuwait.

Katika ujumbe aliomuandikia Emir wa Kuwait Sheikh Sabah al-Ahmad al-Jaber al-Sabah, Rais Rouhani amemkabidhi salamu za rambi rambi kufuatia hujuma ya kigaidi dhidi ya msikiti Mjini Kuwait siku ya Ijumaa na kuelezea matumaini yake kuwa ugaidi utaangamizwa kote duniani.
Rais Rouhani amesema magaidi wa Kitakfiri, ambao wanatekeleza mashambulizi katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, wanalenga kuchafua sura ya Uislamu na kueneza mifarakano na uhasama miongoni mwa Waislamu.
Katika hujuma hiyo ya kigaidi Ijumaa, waumini 27 waliuawa na wengine zaidi ya 220 kujeruhiwa wakati wakiwa katika sala ya Ijumaa ndani ya Msikiti wa Imam Sadiq AS  katika eneo la al-Swabir katika Mji wa Kuwait.../mh

3320493

captcha