IQNA

Imam Khamenei

Hija ni fursa ya kukabiliana na njama za maadui wa Uislamu

21:40 - October 28, 2014
Habari ID: 1465135
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei, amesema kuwa, ibada ya hija ni fursa bora kabisa kwa ajili ya kukabiliana na njama za kuitenganisha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na ulimwengu wa Kiislamu na nara yake ya ‘kukabiliana na shubha na propaganda zinazoenezwa na maadui wa Uislamu’ na kutoa jibu mwafaka kwa mahitaji ya kimaanawi na kifikra za mahujaji.

Kiongozi Muadhamu ameyasema hayo leo Jumanne alipokutana na wasimamiaji wa amali ya Hija ya mwaka 1435 Hijria na kusisitiza kuwa,  ni suala la dharura kuwepo mipangilio mizuri kwa ajili ya utekelezaji bora zaidi wa ibada ya Hija. Ameongeza kuwa, kujaribu kujenga ukuta kati ya taifa la Iran na maeneo mengine ya ulimwengu wa Kiislamu, ni moja ya malengo machafu ya maadui wa umoja wa Waislamu, hivyo ni wajibu wa kila mmoja kuitumia kwa njia bora ibada ya Hija kuvunja ukuta huo bandia na kuleta mabadiliko ya kimtazamo na kuondokana na fikra zisizo sahihi zilizopandikizwa kupitia propaganda za urongo za maadui. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, umoja wa Kiislamu ndilo hitajio la kweli la ulimwengu wa Kiislamu na kufafanua kwamba, umoja na udugu baina ya Waislamu ni katika misingi ya dini tukufu ya Kiislamu na hiyo ndiyo siasa kuu ya Jamhuri ya Kiislamu ambayo katika hilo haimuonei aibu mtu yeyote yule. Akiashiria kuwa, umoja wa Uislamu hauna maana ya kuachana na itikadi za madhehebu za Kiislamu tofauti, amesema kuwa umoja wa Kiislamu ambayo ndiyo nara kuu ya Jamhuri ya Kiislamu, una maana ya kwamba umma wa Kiislamu unatakiwa kutofanyiana uadui kama ambavyo unatakiwa kushirikiana katika mambo muhimu ulimwenguni.../mh

1464905

Habari zinazohusiana
captcha