IQNA

Shughuli za Qur'ani

Walibya waadhimisha Siku ya Kitaifa la Qur'ani

11:44 - November 03, 2022
Habari ID: 3476026
TEHRAN (IQNA) - Programu mbalimbali zilifanyika nchini Libya mapema wiki hii kuadhimisha siku ya kitaifa ya nchi hiyo ya kuwaenzi wnaohudumia Qur'ani Tukufu nchini humo.

Katikati ya mwezi Oktoba, Taasisi ya Qur'ani Tukufu ya Libya iliteua siku ya mwisho ya mwezi Oktoba kuwa siku ya kuwaenzi wanaohudumia Qur'ani Tukufu nchini humo.

Taasisi hiyo ilisema sherehe na program zitakuwa zikiandaliwa kila mwaka katika siku hii, ambayo ndiyo siku ambayo taasisi hiyo ilianzishwa.

Maafisa kadhaa akiwemo Waziri wa Utamaduni na Maarifa wa Libya, Mabrouka Toghy, mkuu wa taasisi hiyo, na wanazuoni, wataalamu na maashiki wa Qur'ani Tukufu walishiriki katika programu za kwanza za aina hiyo siku ya Jumatatu.

Programu hizo zilijumuisha kuwaenzi wanaharakati wa Qur'ani na wale wanaohudumia Kitabu Kitukufu, kutoa hotuba, kutambulisha mbinu za kaligrafia ya Qur'ani, na kutambulisha shughuli za Taasisi ya Qur'ani Tukufu ya Libya.

Mapema mwezi Oktoba, taasisi hiyo iliandaa kongamano la kimataifa kuhusu uandishi wa Qur'ani katika mji mkuu wa Libya, Tripoli.

Taasisi ya Qur'ani Tukufu ya Libya imeanzishwa na Serikali ya Umoja wa Kitaifa (GNU). Imepewa jukumu la kusimamia shughuli za wachapishaji wa Quran, miongoni mwa mambo mengine.

Libya ni nchi yenye Waislamu wengi huko Afrika Kaskazini ambako shughuli za Qur'ani ni maarufu sana. Inasemekana kuwa ina zaidi ya wahifadhi milioni moja wa kuhifadhi Qur'ani Tukufu.

Nchi hiyo imekuwa katika machafuko tangu vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoungwa mkono na NATO mwaka 2011 kupindua na kumuua dikteta mkongwe Muammar Gaddafi.

Libya katika miaka ya hivi karibuni imegawanyika kati ya GNU huko Tripoli, na utawala ulioko mashariki.

4096556

Kishikizo: qurani tukufu libya
captcha