IQNA

Sayyed Hassan Nasrallah

Nchi ziungane kukabiliana na tishio la ugaidi wa ISIS

15:27 - December 10, 2016
Habari ID: 3470732
IQNA: Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amatoa wito wa kuwepo umoja baina ya nchi mbali mbali duniani ili kukabiliana na tishio la kundi la kigaidi la ISIS au Daesh.

Akizungumza Ijumaa usiku kwa njia ya televisheni, Sayyed Hassan Nasrallah ameongeza kuwa kuwa, "Njia pekee iliyoko mbele yetu ni kuulinda ustaarabu wa Kiislamu, eneo na uwepo wetu kwa kukabiliana na ugaidi". Aidha ameashiria kadhia ya Palestina na kuendelea hujuma na ukatili wa utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Waislamu na Wakristo Palestina na kusema: "Waislamu na Wakristo katika eneo wanakabiliwa na tishio kubwa la Israel na magaidi wakufurishaji."

Aidha ameongeza kuwa, nchi za magharibi na hasa Marekani zinaunga mkono kifedha na kisilaha magaidi wakufurishaji na hili ni jambo ambalo hata rais mteule wa Marekani Donald Trump amekiri na pia liko wazi katika email zilizovuja za Hillary Clinton.

Sayyid Hassan Nasrallah amewahutubu watu wanaojaribu kuzusha fitna na hitilafu baina ya Hizbullah na mirengo ya kisiasa ya Lebanon kwa kusema: Wale wanaochimba kisima cha fitna watatumbukia wenyewe kwenye lindi la fitna zao hizo.Katibu Mkuu wa harakati ya muqawama wa Kiislamu ya Lebanon aidha amesema Hizbullah ina uhusiano mzuri sana na Rais Michel Aoun wa nchi hiyo unaotokana na kuaminiana baina ya pande mbili.

Sayyid Hassan Nasrallah ametangaza kwa mara nyingine uungaji mkono wake kwa Michel Aoun na kueleza kwamba uvumi wa kuwepo hitilafu kati ya Hizbullah na Rais wa Lebanon hauna msingi wowote.

Nasrullah amekanusha pia kauli za watu wanaodai kwamba hali ya kisiasa ndani ya Lebanon ni ya wasisiwasi na ya mgogoro na kubainisha kwa kusema, Hizbullah na aliyekuwa Spika wa Bunge Nabih Berri hawajakwamisha mchakato wa uundaji serikali, na kimsingi makundi yote ya kisiasa yanafanya juhudi za kuondoa vizuizi vinavyokwamisha suala hilo na kwamba hadi sasa imebakia nafasi moja au mbili tu za Wizara ambazo bado hazijajazwa.

Kiongozi wa Hizbullah amesisitiza kuwa serikali inapasa kuundwa haraka iwezekanavyo kwa sababu hilo ni kwa manufaa ya nchi; na pande zote zinapaswa kutoa kushirikiana ili kufanikisha uundwaji serikali mpya.

3552363

captcha